Tuesday, January 12, 2016

UVCCM yataka Rais mstaafu wa Zanzibar Dr Aman Abeid Karume Afukuzwe CCM

UVCCM yataka Rais mstaafu wa Zanzibar Dr Aman Abeid Karume Afukuzwe CCM


UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umekitaka chama hicho kumvua uanachama Rais mstaafu wa Zanzibar Dk  Aman Abeid Karume.

Kauli hiyo ilitolewa jana katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Khamis wakati wa kilele cha matembezi ya vijana wa umoja huo kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi.

Alimshushia tuhuma nzito mstaafu huyo kuwa anashirikiana na wapinzani kukihujumu chama hicho kikongwe nchini, na kwamba asipofukuzwa umoja huo utatumia njia zingine ambazo hakuziweka wazi.

Sadifa alionya kwamba Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar si mali wala miliki ya mtu kwani Wazanzibar wote wana haki ya kushiriki kuyaenzi kwa vitendo kutokana na historia yake.

No comments:

Post a Comment