Friday, January 8, 2016

MANJI AINGIA KWENYE TASNIA YA HABARI KWA KUNUNUA GAZETI LA JAMBO LEO

Manji Alinunua Gazeti la Jambo Leo



Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania ambao ni wachapishaji wa Gazeti la kila siku la Jambo Leo imenunuliwa na Kampuni ya Quality Media Group ambayo ni kampuni tanzu ya Quality Group Limited,ununuzi umeanza December 31 na unategemea kukamilika February 01.

Kampuni ya Quality Media imedhamiria kuwekeza katika tasnia ya habari kwa kuongeza ufanisi katika utendaji wa gazeti la Jambo Leo na kuahidi kufikia mwisho wa robo ya kwanza ya mwaka 2016 kuongeza machapisho mengine ikiwa ni pamoja na gazeti la kiingereza la kila siku na gazeti toleo la wiki la Afrika Mashariki.

Mkurugenzi mtendaji wa Quality Group, Bw. Arif Sheikh alisema: “Kampuni ya Quality Group imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Jambo media inakuwa chombo cha habari bora na cha kuaminika nchini Tanzania na katika ukanda wote wa Afrika Mashariki”

“Tumedhamiria kuhakikisha kunakuwepo na uhuru, uwazi na ukweli katika utoaji taarifa ili kuhakikisha umma unaarifiwa habari za uhakika,” aliongeza.

“Hivi punde tutatangaza bodi ya ushauri ya uhariri (Editorial Advisory Board) kwani kama wanahisa, tusingependa kuingilia maadili ya kiuandishi,” alimalizia.

No comments:

Post a Comment