CHAMA
cha Wananchi CUF kimeitisha vikao vya juu vya kitaifa vya Chama ili
kujadili marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliotangazwa kurudiwa
Machi 20, 2016 na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Katika
taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa
CUF, Ismail Jussa, imesema kuwa vikao hivyo vitafanyika Januari 27 na 28
mwaka huu, na ndivyo vitakavyotoa msimamo rasmi wa CUF.
Ifuatayo ni taarifa kamili ya Jussa.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kufuatia
tangazo jengine la kihuni lisilozingatia Katiba wala Sheria la
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha
kutangaza tarehe 20 Machi, 2016 kwamba ni siku ya kile anachokiita
uchaguzi wa marudio Zanzibar, Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitisha vikao
vya juu vya kitaifa vya Chama ili kujadili suala hilo na kutoa msimamo
rasmi wa Chama.
Kamati
ya Utendaji ya Taifa itakutana Jumatano, tarehe 27 Januari, 2016 na
kufuatiwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litakalokutana Alhamis,
tarehe 28 Januari, 2016. Vikao hivyo vitafanyika Ofisi Kuu ya Chama,
mjini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment