Diamond Platnumz: Baada Ya Nape Nnauye Mimi Ndo Waziri wa Habari Na Michezo Mtarajiwa
Diamond
Platnumz amesema akiachana na muziki anataka kuwa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuweka vitu sawa na kutoa fursa zaidi
kwa vijana.
Akizungumza
katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Diamond alisema kama akiingia
kwenye siasa basi nia yake ni kuwa Waziri wa Michezo.
“Kwa
sasa hivi siasa bado ila nikiingia kwenye siasa baadaye akimaliza
mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo,” alisema na kuongeza;
“Kile
nakiweza kabisa kwa sababu mimi ukinimbia sijui kuhusu mpira, movie
mimi naweza kabisa nikiwa Waziri, nikavifanya na vikawa na maendeleo.
"Ni
kitu ambacho naweza siyo nasema nataka kuwa mbunge ila mimi nataka ile
siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye siasa basi nakuwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuboresha vitu”
No comments:
Post a Comment