kudumisha mapenzi katika ndoa
Katika kujadili mada hii nyeti
ambayo inagusa maisha ya kila mmoja wetu kwa kiasi kikubwa nitaijadili katika
sehemu kuu tatu. sehemu ya kwanza ya utangulizi kwa ufupi nitaangazia maana ya
mapenzi na ndoa kwa ujumla sehemu ya pili nitaangazia vitu vipi vya kuzingatia
kabla ya kuingia katika mahusiano na mtu katika ndoa.
Sehemu ya tatu nitaangazia ni
yapi baadhi ya mambo yanayopelekea kushuka kwa mapenzi katika ndoa na sehemu ya
mwisho nini kifanyike kuendeleza mapenzi katika ndoa.
Neno Mapenzi ni neno ambalo
lina tafsiri nyingi na Kila mtu ukimuuliza atakupa maana yake aijuayo
kulingana na mtizamo wake. lakini kwaufupi naweza kuelezea mapenzi baina ya
wapenzi kama ukaribu unaowaunganisha jinsia mbili tofauti yaani jinsia ya kike
na kiume pamoja kwa hisia za kimahaba.
Neno Ndoa naweza kuelezea kama taasisi kongwe ambayo ilianzishwa na
mungu mwenyewe pale edeni alipowaunganisha adamu na eva. Ndoa hutokea pale
ambapo wapendanao wawili wanapoamua kurasimisha mahusiano yao kulingana na
taratibu za kimila kijamii kidini na kisheria. Wawili hawa wanaamua kwa hiari
yao kuwa mwili mmoja na kuishi pamoja hadi pale kifo kitakapowatenganisha.
baada ya kuelewa maana ya mapenzi
na ndoa sasa tunaweza kuelewa jinsi gani ya kudumisha mapenzi katika ndoa.
Kwanza kabsa kuna vitu vya msingi ambavyo unatakiwa uvifahamu kabla ya kuingia
katika ndoa ili kuwa na ndoa bora na uwe na uwezo wa kudumisha mapenzi katika
ndoa.
Kwanza yapasa uwe umefanya uamuzi
sahihi yakuwa unataka kuingia kwenye ndoa usiingie kwenye ndoa kwa kulazimishwa
na mtu yeyote ama kwa kufuata mkumbo
Pili uwe umefanya uchaguzi sahihi ya mtu
ambaye unataka kuishi nae katika ndoa. Hakikisha umeielewa tabia yake vizuri na
kwamba utaweza kuendana nayo.usioane na mtu kwa tamaa ya vile vitu ambavyo
anamiliki.Hakikisha kweli umempenda na unakuvutia pia kuwa naye.
Tatu umuelewe kipi amependa kwako
kama ni uzuri wako au pesa zako au umaarufu wako. Hii itakusaidia katika kujua
kiwango cha upendo wake kwako na uhalisia wa upendo wake kwako.
Mbali na hayo lakini pia uwe na
uelewa kuwa katika maisha ya ndoa kuna wakati mtaingia katika migongano hii
itakusaidia jinsi gani ya kukabilina nayo.
Hayo ni baadhi ya mambo ya msingi
ambayo wapenzi wanatakiwa kuyazingatia kabla ya kuingia katika ndoa. Baada ya
kujadili hayo hebu sasa tuone vitu gani vinaweza kudumaza mapenzi katika ndoa
na kuyafanya yasiendelee kukua na kuwa ya furaha bali kupoteza radha na mwisho
wake kusambaratika.
Kuzoeana.. Kunawakati unafika
wanandoa wanakuwa wanafahamiana vyakutosha kutokana na kuishi mda mrefu. Hii
hupelekea watu kuonana wakawaida kisi kwamba mahaba kati yenu yanaondoka. Hili
laweza kwenda mbali zaidi hata kutoshiriki vizuri haki ya ndoa kama zamani
kwani mshapoteza mahaba.
kupoteza mvuto; Ikumbukwe kuwa
wakati mna kutana kwa mara ya mwanzo katika uchumba kuna vitu ambavyo kila
mmoja vilimvutia kwa mwenzie mfano usafi au umaridadi, tabasamu maumble mfano
unene au wembamba, rangi mfano nyeusi au maji ya kunde. Hivi vikija kupotea
wakati mkiwa kwenye ndoa inachangia kudumaza mapenzi. Mfano kabla hamjaona na
mumeo ulikuwa msafi unaoga marakwa mara unanukia marashi na kujipamba hii tabia
ikipotea mvuto wako kwa mumeo unapungua na hatari yake huathiri upendo wa mumeo
kwako.
Tabia ya ubishi na ukiburi pamoja
na ujeuri.. Unapokuwa mtu ambaye hutaki kuwa tayari kumsikiliza mwenzio anataka
nini ,anapenda nini na nini hapendi unamfanya mwenzio awe anakasirika
marakwamara kwani una muudhi muda wote mwisho wa siku anakupuuzia na athari
yake ni kupoteza mapenzi katika ndoa.
Kutokuwa mwaminifu katika ndoa..
Mmoja wa wanandoa anapokosa uaminifu na kuanza kujihusisha na wapenzi wengine
mbali na mumewe au mkewe kunapunguza mapenzi katika ndoa. penzi la nje mara nyingi linamlevya mtu na
kumfanya aone mkewe au mumewe si kitu. Pia kutokuwa mwaminifu pindi ufumaniwapo
na mwenzi wako unapoteza mapenzi yake kwako.
Nini sasa kifanyike ili kudumisha
mapenzi katika ndoa?.
Kwanza yapasa kudumisha urafiki
katika ndoa. Msiache kutendeana kama mlivyokuwa mwanzo kabla hamjaoana.
Jua mwenzio nini hapendi na nini
anataka. Usifanye yale yote ambayo ni kero kwa mwenzio.
Heshima kwa kila mmoja wenu ni
muhimu. Muheshimiane kwa kila jambo na msikaribishe dharau kati yenu.
Kila mmoja ajue nafasi yake
katika ndoa. Mwanamke ajue yeye ni msaidizi na kazi yake ni kumshauri mume. Na
mume awe anacheza nafasi yake na majukumu yake kama kichwa cha familia. Akubari
ushauri toka kwa mkewe na asimdharau mke.
Uaminifu katika ndoa ni jambo
muhimu sana kwani mume au mke anapojua mwenziwe ni mwaminifu huongeza nguvu ya
mapenzi katika ndoa kuliko akijua kuwa mwenzie si mwaminifu.
Kujipamba na swala la usafi kwa
mwanamke ni jambo jema sana. Hili
huchochea mvuto kwa mwanaume na kuongeza chachu ya mapenzi. Ni ukweli
usiofichika kuwa wanaume mara nyingi huvutiwa zaidi na mwanamke masfi anaye
jipenda na kujipamba.
Swala lingine muhimu ni mambo ya
ndani ya kindoa zaidi. Hapa namaanisha swala la kupeana haki ya kindoa(Tendo la
ndoa) . Wana ndoa wanapaswa kuridhishana ki uhakika kwani mapungufu katika eneo
hilo huchangia kwa kiasi kikubwa mapenzi kuharibika.
Swala kumshirikisha mungu pia ni
jambo la kuzingatia. twapasa kukumbuka kuwa mungu mwenyewe ndie mwanzilishi wa
mapenzi na ndoa. Ndiye yeye aliyefungisha ndoa ya kwanza kati ya adamu na eva.
Hivyo swala la ibada na kumwomba alinde mahusiano yenu ni muhimu sana.
ubunifu katika mapenzi ni jambo la msingi.
Kuishi pamoja nayo ni changamoto hivyo inabidi uwe mbunifu wa kukufanya uwe
mpya kilasiku ili mpenzi wako asikuchoke. Vitu kama kupeana zawadi ni muhimu kwa
wapenzi hasa katika ndoa isiishie tu kipindi cha uchumba. Kutoka kidogo sehemu
za starehe maramojamoja ni muhimu pia kwani mnapata wasaa wakutazamana vzuri na
kuvutiana na kuzungumza mambo yenu.
Kusifiana pia ni muhimu hatakama
linaonekana jambo dogo. Mtu akisifiwa hujisikia kukubalika hivyo humpa furaha.
Mpe sifa mkeo pale anapovaa vzuri au anapofanya kitu kizuri. Kiasiri wanawake
wanapenda kusifiwa juu ya urembo wao hivyo huwapenda wanaume wenye uwezo wa
kusifia.
Swala la kuomba msamaha wakati
ukiwa umekosea ni la msingi. Wanaume wengi huwa wanashindwa sana hili eneo na
hii ni kutokana na mfumo dume uliowakuza katika jamii. Niwazi kuwa kila mtu
anakosea na kuomba msamaha ni lazima na kusamehewa ni haki yako. ukiburi wa
kutoomba msamaha ni chachu ya kurudia
kosa kwa mara nyingine na kusababisha makwazano katika ndoa ambayo hupelekea
uharibifu wa mapenzi katika ndoa.
Kwakweli somo la kudumisha
mapenzi katika ndoa ni zito na ni refu
sana yapasa kila siku wanandoa kujifunza. Kujifunza ni kwa aina nyingi sana ,
waweza kukaa na wazee waliokaa kwenye ndoa muda mrefu watakueleza siri
mbalimbali za ndoa na watakupa uzoefu wao ambao utajifunza mengi. Zingatia
maisha yako yanaweza kuwa mazuri kama utakuwa na ndoa yenye upendo na amani na
furaha. Pia maisha yako yanaweza kuharibika na kuwa machungu kama utakuwa na
ndoa chungu na isiyo na furaha.
Imeandikwa na Richard priva Zalala
Email. Richard.priva@gmail.com
No comments:
Post a Comment