Sunday, January 17, 2016

DIAMONDPLATINUMZ AKA SIMBA AZIDI KUNG’ARA YOUTUBE.





 

Msanii Nasibu Abduli  ama Chibu Dangote anazidi kufanya vizuri kila iitwapo leo katika sanaa ya muziki. Katika kipindi kifupi cha maisha yake katika sanaa ameweza kufanya makubwa sana ambayo watangulizi wake hawakuweza kuyafanya. Mbali na kubeba tuzo mabalimbali za heshima ndani na nje ya nchi hadi kufikia hatua ya kujiita mond bin awards Diamond amekuwa msanii wa kwanza East Africa kupata views zaidi ya million moja kwenye mtandao wa youtube.Nyimbo yake mpya ya utanipenda  hadi sasa ishafikisha views milioni mbili .
Hebu angalia video zake zilivyopata views nyingi
1.Diamond feat Davido, number one remix ,12 million views
2.Diamond feat mr flava nana ,8 million views
3.Diamondplatinumz ,nitampata wapi , 7milion views
4.Diamondplatinumz nasema nao  6million views
5.Diamond ,mdogomdogo  5 million views.
Idadi ya watazamaji wa video zake katika youtube inakuwa kubwa kutoka na kuipenda kazi yake na kujituma kwa bidii kubwa. Pia Diamond amekuwa msanii ambaye anajua kuwekeza hela katika mziki wake. Anatumia pesa nyingi kurekod video nzuri na ma director wakubwa kama kina Godfather wa South Africa yote ni kutaka kupata kazi nzuri. Maoni yangu kwa wasanii wengine mfuate mfano huu mkuze mziki wetu.
By Richard priva zalala
Email.richard.priva@gmail.com




No comments:

Post a Comment