ELIMU BURE NI NZURI LAKINI YAFAA ITAZAMWE VIZURI
Na mchambuzi wako Richard priva zalala
Ningependa kuchukua nafasi hii kuipongeza serikali kwa
jitihada inazozichukua katika kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya
elimu.
Kama tujuavyo swala la elimu ni jambo muhimu sana kwa
maendeleo ya uchumi wa nchi yoyote
duniani.
Mataifa makubwa duniani kama Marekan,Uingereza na China
yameweza kuwekeza vizuri katika elimu ambayo imechochea kukua kwa teknolojia
Kafka nchi hizo .Kukua kwa teknolojia kumepelekea ukuaji mkubwa wa uchumi
katika nchi hizo. Hivyo ni naweza kusema kuwa pasipo kuwekeza katika elimu taifa
haliwezi pata maendeleo yoyote.
Historian ya utoaji was elimu nchi hii baada ya kupata uhuru
ilikuwa ni utoaji wa elimu kwa wananchi pasipo kutozwa mojakwamoja. Bali kodi
za wananchi zilizo kusanywa ndizo zilitumika kugharamia elimu. Wanafunzi enzi
hizo walikwenda mashuleni na kupata vifaa vya shule kama daftari na kalamu .
Miaka ilivyoendelea ikaletwa Sera ya kuchangia huduma yaani cost
sharing ili kuipunguzia mzigo serikali na wanachi kuchangia katika
gurudumu la maendeleo ya nchi.
Kutokana na wazazi wengi hasa wa vijijini kuwa na hali ngumu
ya kiuchumi serikali ilipinguza ada. Kutoka elfu arobaini hadi elfu ishirini
kwa sekondari za kutwa na elfu sabini kwa shule za bweni.
Mbali na kupunguza ada lakini bado wazazi walipata mzigo
mkubwa kuchangia michango mbali mbali ambayo kimsingi ilizidi hata ada za
shule.
Mfano w michango hiyo ni
Dawati taluma, tahadhari, rimu , chakula kwa shule za kutwa
ambazo wanafunzi walikua wanakula mashuleni.michango ya maabara na ujenzi wa madarasa.
Mbali na hapo wanafunzi wa bweni walihitajika kugharamia
mchango wa umeme walitakiwa pia wawe na vifaa kama majembe mafyekeo pamoja na mashuka magodoro ,ndoo
na sanduku la chuma la kuhifadhia vifaa vyao. Ukipiga Mahesabu vitu vyote hivyo
utapata gharama kubwa sana kumpa mzazi
mzigo mkubwa.
Hii iliwapekekea wazazi wengi washindwe kumudu ghaeama za
kusomesha na wengi wao wakafikia hatua ya kutowapeleka watoto shule. Wengine
walidiriki kuwaambia watoto wao wasifanye vizuri mtihani ya mwisho wa darasa la
saba kuingia kidato cha kwanza.
kwa shule za msingi hasa za mijini wanfunzi walilazimishwa
kubeba pesa za twisheni na mitihani ya kila wiki .
Faida za elimu bure.
Ø Elimu pasipo malipo itawsaidia wazazi
wengi kuwapeleka watoto wao shule kwani wamepunhuziwa mzigo mzito wa ada na michango mashuleni
Ø Wanafunzi waliokuwa wanashindwa kipa
ada za mitihani ya taifa hadi kupekekea kufungiwa matokeo yao sasa hawatapatwa
na kadhia hiyo tena.
Ø Idadi ya wanafunzi kwenye shule za
sekondaei itaongezeka kwani wazazi hawana tena kisingizio cha kutowapeleka
shule watoto.
Ø Serikali itakua imefikia malengo take
ya kuwawezesha watoto wengi wa kimasikini kupata elimu ya sekondari ambayo ni
muhimu kwa maisha yao na maendekeo ya nchi kwa ujumla.
Ø Kuzibwa kwa mianya ya ufisadi uliokua
ukifanywa mashuleni na walimu wa kuu pamoja na bodi za shule kwa kutumia vibaya
michango ya madawati ,taaluma na ujenzi wa madarasa.
Changamoto za elimu
bure
Japo serikali kwania njema imeamua kutoa elimu bure kwa
wanachi wake lakini mpango huu kwanamna Moja ama nyingine unakabiliwa na
changamoto nyingi.
Kwanza pesa ambazo zinapelekwa mashuleni kama fiidia ya ada
na capitation grant ni kidogo ukilinganisha na matumizi ya shule
Shule nyingi zimeajili wafanya kazi kama walinzi ambao wanatakiwa
walipwe kila mwezi .Matumizi ya maji na umeme ,shule sasa zinatakiwa kulipia
mitihani ya ndani na ile ya kikanda kama moko ambayo hapo kabla wanafunzi
walikuwa wanachangia. Halafu utakuta shule imepewa laki saba,.nane hadi milioni
nakupangiwa matumizi yote mfano kuchapa mitihani, kulipa walinzi,matengengenezo
madogomadogo kulipia maji , umeme.
Ambapo ukiangalia
kiuhalisia she kwa mzwezi matumizi ya shule ni makubwa kuliko hizo pesa.
Mfano shule nyingi za sekondari zina uhaba wa walimu wa
sayansi hivyo zimeajili walimu wa masomo hayo wa part time kwa kutumia michango
toka kwa wazazi. Serikali kwa kukataza
michango halafu inatoa pesa kidogo maana take ni kuwa shule zitashindwa kuwalipa
walimu hawa na matokeo yake wanafunzi watashindwa kusoma masomo haya.
Changamoto nyingine ni kuwa walimu ambao nao ni wadau wakubwa
wa elimu hawajafikiriwa. Mazingira ya kufundishia ni mabovu. Walimu hawalipwi
stahiki zao mfano hawapandishwi madaraja kwa wakati hawapewi pesa zao za likizo
wana malimbikizo makubwa ya madeni wanayoidai serikali.hivyo katika lengo la
serikali la kuboresha elimu itakua vigumu kwakua watoaji wa elimu hiyo hawana morali ya kufanya kazi.
Mishahara midogo hawan nyumba za kjishi wala posho za nyumba
hawana posho kama katika kada zingine za utumishii
Maoni
Serikali katika kuboresha elimu inapaswa iangalie pande zote
yaani wanafunzi wazazi na walimu .
Kero za walimu zitatuliwe ili walimu wafanye kazi kwa bidii
na kuweza kuinua kiwango cha elimu. Serikali iache siasa katika elimu isiwe inaingilia sana taaluma hii kwa kufanya
maamuzi yaliyoelemea kujinufaisha kisiasa. Wanasiasa na watumishi waliopewa dhamana
ya kusimamia elimu na walimu waache kuwanuanyasa walimu na badala yake wajikite
katka kutatua kero zao.
Pia serikali iongeze uwekezaji katika elimu kwa maana kiwango
kinachowekeza sasa katika elimu ni kidogo ukilinganisha na uhitaji uliopo.
Na Richard priva
zalala
Email Richard.priva@gmail.com
No comments:
Post a Comment