DOMESTIC VIOLENCE
KATIKA MAHUSIANO NA WIVU ULIOPITILIZA KIWANGO.
Naweza kuelezea domestic violence
kama ghasia zinazo ambatana na unyanyasaji katika mahusiano ambao unafanywa na
mmoja wapo wa mwenza katika mahusiano ili kumtawala mwenziwe. Unyanyasaji huu
unaweza kumtokea yeyote bila kujari rangi, kabila , umri wala jinsia.
Unyanyasaji huu unaweza kuwa wa aina mbalimbali mfano kumuumiza mtu mwili wake,
unyanyasaji wa kingono kiuchumi na kisaikolojia. Domestic violence yaweza
kuhusianisha wapenzi wote wawili kwa maana nyingine ya kiingereza inaitwa
reciprocalviolence ambapo wapenzi wote ni wakorofi. Pia yaweza kuwa si wapenzi
wote ambao ni wakorofi bali mmoja kati yao ndio mkorofi kwa kiingereza nonreciprocal violence ambapo mmoja wa
wapenzi ni mkorofi.
Kuna aina mbalimbali za domestic
violence ambazo hutokea katika mahusiano ya mwanaume na mwanamke katika jamii
kwa mfano.
Kudhuru mwili(physicalabuse) .Hii
huusisha mmoja kati ya wapenzi wawili kumsababishia mwenziwe maumivu ya mwili
mfano kwa kumpiga ,kumchoma na vitu vya ncha kali au visu, kuunguza kwa moto au
maji ya moto, kujeruhi kwa vitu vizito.
Kumlazimisha mtu ngono
(sexualabuse).Huu hutokea wakati mmoja anapomlazimisha mwenzie ngono wakati
hayupo tayari kwa kitendo hiko
Kumuumiza mtu kisaikolojia(psychological
abuse).Hii inajumuisha kumnenea mtu maneno makali ya vitisho, kumshusha mtu
thamani yake mfano kumtishia mwenza kifo kama atajaribu kuvunja mahusiano.
Kumdhalilisha menzio mfano kwa kumtukana
Unyanyasaji wa
kiuchumi(economicabuse).Huu hutokea wakati mmoja wa mwenza anapojaribu
kumdhibiti mwenzie katika Nyanja ya uchumi na kumfanya asiwe na uwezo wowote
kiuchumi na kumtengenezea mazingira ya utegemezi kwako.mfano kuna wanaume wana
waachisha wake zao kazi au kuwazuia kabisa kufanya kazi kisa tu wakizani
wakizani mwanamke akiwa na kazi huwa kiburi. Na wengine ni sababu za wivu tu
anahofia bosi au wafanyakazi wenzake watamchukua.
Kuna sababu mbalimbali ambazo
zimekuwa chanzo cha domestic violence katikati ya wapendanao moja ya sababu
kubwa ni wivu uliopitiliza kiwango. Ningependa tujadili swala la wivu kwa
mapana na marefu katika kuchangia kwake katika ghasia ambazo hutokea katikati
ya wapenda nao.
Wivu unahusisha hisia na mawazo
hasi na hisia za kutojisikia usalama, hofu wa kumpoteza mtu ambaye unamthamini
sana hasa mpenzi. Wivu umekuwa ni jambo la kawaida katika mahusano na hakuna
awezaye kulepuka ila tunajaribu kulidhibiti lisilete madhara. Wivu ni daliali
moja wapo ya kuonyesha mtu kama ana mpenda mwenziwe. Wivu uliopitiliza kiwango
sio alama ya mapenzi ya dhati kwa mwenzi wako bali ni ugonjwa au udhaifu ambao
unaitaji kuupatia tiba.Wivu uliopitiliza huu ni wivu ambao uko tofauti sana na
wivu wa kiasi. Tofauti yao ni kwamba huu huleta madhara kwa mmoja wa wapenzi
pasipo kuwa na sababu zenye mashiko.
Wivu uliopitiliza husababishwa na mtu
kutokujiamini na kutomuamini mwenza wako ukifikiri muda wowote anaweza
kukusaliti.
Wakati mwingine hutokea kwa hisia
tu zako binafsi kuhisi kama unasalitiwa au yaweza
tokea pale mmoja wa wapenzi anapokuwa anaanza kuonyesha tabia ya kutokuwa muaminifu.kwa mfano mpenzi wako
anapoanza kukuhisi au kuwa na ushahidi kuwa una mahusiano mengine yasiyo rasmi
mbali nay eye anaweza kuanza kuwa na wivu liopitiliza.
Kutokujiamini kama unavutia. Wakati mwing imekuwa ikitokea mmoja wa
wapenzi anasikia wivu mkali anapomuona mpenziwe yupo karibu aidha kikazi au
kibiashara au hata kwa ujirani mwema na hasa anapozani kuwa huyo mtu ni mzuri
kuliko yeye. Hii hutokea hasa kwa wanawake huwa wanakosa amani na kuwa na wivu
mkali sana.
Hofu ya kuachwa pia
huchangia,Kuna wakati aidha mwanamke au mwanaume unapokuwa umempata mwenza
ambaye pengine hukutegemea kumpata maishani hivyo unaona kana kwamba ni bahati
kuwa naye. Au yawezekana ulikaa muda mrefu bila kuwa na mpenzi na sasa
umempata. Kutokana na hivyo basi unakuwa
na wivu sana juu ya mpenzi wako kwakuhofu ya kumpoteza .
Wivu uliopitiliza hujidhiirisha
katka namna mbali mbali mfano kujaribu kumdhibiti mwenza wako katikamambo
mbalimbal mfano kumchagulia mwenza wako watu wa kuongea nao wakati mwingine
hata kwa watu wasio na madhara yoyote kwa mahusiano yenu mfano ndugu.
Kupekuapekua simu ya mwenza wako
kila mara kutaka kujua amewasiliana na nani.
Tabia ya kugombezana mara kwa
mara mfano mwanamke akichelewa dukani hata kwa sababu za msingi au mwanaume
kuchelewa kuludi kazini. Kuchelewa pokea simu.
Wivu uliokithiri una madhara
makubwa kama tulivyo jadili awali kuwa hupelekea ghasia bana ya wapenzi kati ya
wapendanao na ghasia hizi hupelekea matukio mabaya kama Vipigo na kuumizana . mmoja katika
mahusiano mwenye tatizo la wivu uliokithiri hujikuta akimuumiza mwenziwe na
hata kumpotezea mwenzie maisha.si jambo gani kuhusikia mtu amechoma kisu mumewe
au mkewe kwa sababu ya wivu wa mapenzi au hata kumuumiza mtu anaye mshuku
kumchukulia mpenzi wake.
Kujihusisha na maswala ya
kishirikina kwa wale waaminio ushirikina. Ukitembea mitaani utaona mabango
mengi ya waganga wa jadi yakiwanadi kuwa wana uwezo wa kumtuliza mpenzi na
kumfanya akupende wewe. Mwenye wivu uliokithiri kwasababu saa zote hajiamini basi
ata tafuta njia za kumdhibiti mwenza wake ikiwemo hii ya waganga wa kienyeji
kwa wale wanoamini mambo haya. Mwisho wake wanajikuta wanapoteza pesa ,muda na
madhara mengine mengi.
Kuleta utengano katika
mahusiano mahusiano kwani uhusiano
unakuwa sio wa furaha na amani. Matukio ya kupigwa kutukanwa abnampelekea mmoja
wa penzi kuchoshwa na mwisho kuamua kuvunja mahusiano
Wivu uliokithiri husababisha mtu
kukonda kwakuwa anakosa amani muda wote anamuwaza mwenzi wake.anafikia wakati
anatamani amuone kila anapoenda na amjue kila mtu anayeongea nae na kukaa nae.
Kutokana na ukweli kuwa wivu u
liokithiri huleta madhara makubwa inabidi tuchukua tahadhari ya kuuepuka. Una
uwezo mkubwa kabsa wa kuumaliza wivu wako. Chakwanza lazima ujiamini kuwa
mpenzi wako haukumpata kwa bahati na kuwa anakupenda .uaminifu ni muhimu kwani
utakufanya ujisikie salama wakati wote hata pale mwenzi wako anapokuwa mbali na
wewe.
Kama mwenzi wako unajua ana
tatizo la wivu inabidi ujaribu kuondoa na kuacha mambo yote ambayo yatamfanya
asijiamini na kutokuamini. Mfano kuongea na simu na watu wa jinsia tofauti muda
mwingi na mara kwa mara, kupokelea simu bafuni au mbali naye na kuongea kwa
siri.
Acha tabia ya kumchunga sana
mwenza wako na kutompa uhuru wa kufanya mambo yake mfano kufatilia sana simu
yake kwani kufanya hivyo ni mazingira ya kuanza kujitengenezea wivu
uliokithiri. Kama mtu nafanya mambo
kinyume na mahusiano yenu lazima utagundua lakini si kwa kujaribu
kumchunga.amini kwamba yeye ni mtu mzima anaweza akajichunga yeye mwenyewe.
Jaribu kujidhibiti kidogo katika
kupenda kwako usipende kupitiliza, kupenda bila kiasi huchangia sana kuwa na
wivu mkali na mwisho wa siku unakusababishia madhara.mpende mwenzi wako vile
inavyotatikana kwani kila jambo ukilifanya bila kiasi mwisho wake huwa si
mzuri.
Imeandikwa na Richard Priva Zalala
Email. Richard.priva@gmail.com
Facebook. Richard priva Zalala
Instagram. Priva29
No comments:
Post a Comment