Serikali Yakubaliana na Hoja ya Zitto Kabwe......Yauondoa Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano Bungeni
Serikali
imeamua kuondoa hoja yake ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano
iliyokuwa imeuawasilisha mapema leo bungeni baada ya kudaiwa kuwa
kilichowasilishwa hakikuwa mpango wa miaka mitano bali mwelekeo wa
mpango wa mwaka mmoja.
Hatua hiyo imefikiwa
baada ya wabunge Tundu Lissu na Zitto Kabwe kupinga mjadala wa hoja
hiyo katika kikao cha leo mchana kuwa hakuna haja ya kuendelea na
mjadala hadi serikali ipeleke mpango wa miaka mitano ukiambatana na
muswada wa sheria husika.
Katika
kikao hicho, ilipelekea mwenyekiti wa bunge Andrew Chenge kuahirisha
kikao baada ya kambi ya upinzani kugoma kutoa maoni yake kupitia kwa
mbunge David Silinde, na kupangwa kikao hicho kingeendelea jioni.
Katika kikao cha jioni, Mwenyekiti wa bunge alilazimika kuahirisha bunge hadi Jumatatu ijayo baada serikali kukubali kuondoa hoja yake kwa ajili ya kujipanga upya.
No comments:
Post a Comment