.....Asema Ndani Ya Miaka Miwili Hakuna Mwanafunzi Atakaye Kaa Chini Kwa Kukosa Dawati
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
George Simbachawene amesema atahakikisha shule zote hapa nchini zinakuwa
na madawati yanayofanana.
Alisema
hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari kuzungumzia
changamoto za elimu bila malipo iliyoanza kutolewa Januari mwaka huu.
“Katika
historia ninayotaka kuandika ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa
chini katika kipindi cha miaka miwili lazima tuondokane na tatizo hili,” alisema na kuongeza kuwa atakuja na ubunifu utakaoondoka tatizo hilo nchini.
“Nataka
kuwe na madawati yanayofanana nchi nzima yenye lebo ya For Government
Primary School, ninaona mwanga mkubwa mbele yangu na katika hili
ninaweza kufanikiwa nipeni fursa,” alisema.
Alisema
pia kumekuwa na changamoto kubwa ya matumizi ya fedha zilizopelekwa kwa
ajili ya kugharamia elimu na kuongeza lengo la serikali kutoa elimu
bila malipo litabaki pale pale kwani miaka ya nyuma watoto wengi
walishindwa kupata elimu kutokana na gharama kuwa kikwazo kwao.
Simbachawene
alisema changamoto kubwa ni kwa walimu kudhani fedha zilizopelekwa
shuleni ni za mwaka mzima lakini ukweli ni kuwa fedha ni za kila mwezi.
Alisema
kila mwanafunzi wa shule ya msingi ya serikali atatoa shilingi 10,000
na kwa sekondari ni shilingi 25,000 kwa mwaka kwa ajili ya uendeshaji wa
shule.
Waziri
huyo alisema kwa shule za sekondari za kutwa kila mwanafunzi atapata
shilingi 3,540 na kwa shule ya sekondari ya bweni ni shilingi 7,243.
“Ukiwa
na wanafunzi 500 maana yake shule inapata zaidi ya shilingi milioni 3.6
kwa mwezi mmoja tu je ukipata fedha hizo unashindwa kuendesha shule?”
alisema na kuongeza kuwa serikali pia ilipeleka fedha za chakula ili
watoto waweze kula lakini fedha hizo zisitumike kulipa madeni ya samani
ya wazabuni.
Aliwataka walimu wasivunje moyo juhudi zinazofanywa na serikali kwani mzazi masikini amepokea mzigo mzito sana na serikali.
No comments:
Post a Comment