Wanayakana makubaliano ya awali yaliyotolewa mahakamani
na
aliyekuwa wakili wake
Dar es
Salaam. Mvutano kati ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutaka
kubomoa nyumba anayoishi Mchungaji Getrude Rwakatare umezidi kushika kasi
mahakamani.
Hali hiyo
ilitokea jana, baada ya wakili wa familia ya Mchungaji Rwakatare, Emmanuel
Agustino kupinga maombi ya NEMC ya kutaka kuongezewa muda wa kuwasilisha maombi
ya mapitio ya hukumu ya maridhiano inayozuia baraza hilo kuchukua hatua yoyote
dhidi ya nyumba hiyo.
Hukumu
hiyo ya maridhiano ilitokana na kesi iliyofunguliwa 2012 katika Mahakama Kuu
Kitengo cha Ardhi na Robert Brighton, ambaye ni mtoto wa Mchungaji Rwakatare
aliyepinga kubomolewa kwa nyumba hiyo kwa madai kuwa imejengwa mahali
pasiporuhusiwa.
Hukumu
hiyo ilitolewa na Jaji Hamisa Kalombola Mei 11, 2015, pamoja na mambo mengine,
alisema pande zote zilikubaliana kuwa, NEMC na wadau wake wasimbughudhi
Brighton katika makazi hayo.
Hata
hivyo, Desemba 29, 2015, NEMC ilifungua tena maombi ya kutaka kupatiwa kibali
cha kuongezewa muda wa kuwasilisha maombi ya kufanya mapitio ya hukumu hiyo.
Katika
maombi hayo namba 825 ya mwaka 2015, NEMC inadai kutoitambua hukumu hiyo na
kwamba, uamuzi huo ulifikiwa na mwanasheria wake ambaye hakupatiwa idhini na
NEMC.
Hata
hivyo, wakati maombi hayo yalipotajwa mahakamani hapo Jumatatu wiki hii, Wakili
Agustino kwa niaba ya mjibu maombi (Brighton), aliwasilisha hati ya kiapo
kinzani dhidi ya hati ya kiapo cha NEMC kilichoapwa na Mkurugenzi wake
Mtendaji, Bonaventure Baya akipinga maombi hayo ya NEMC.
Jaji
John Mugeta anayesikiliza shauri hilo, aliamuru watoa maombi wawasilishe
mahakamani hapo majibu ya kiapo kinzani cha mjibu maombi kabla ya Januari 20 na
akapanga kusikiliza maombi hayo Januari 21, 2016.
No comments:
Post a Comment