MBUNGE
wa Nzega Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein
Mohammed Bashe amejitokeza hadharani na kumtaka Waziri wa Zamani wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe kuacha kulipotosha taifa kutokana kauli zake juu ya
utendaji wa Rais John Magufuli.
Hivi karibuni, Membe alikosoa hatua
mbalimbali zilizochukuliwa na Rais Magufuli. Pia, alipinga hatua ya
kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.
==>Kupitia ukurasa wake wa facebook, Bashe ameandika;
Membe Amuache Ndg Magufuli Afanye kazi.
Membe
amekua waziri for ten yrs ametimiza wajibu wake amuache Ndg Magufuli
atimize wajibu wake. Aliomba Urais Hajateuliwa asubiri 2020 or 2025 ili akipita aanzishe uvasko dagama tena.
Hoja kuwa serekali haijapungua ama kubwa au ndogo ama hoja kuwa Safari za nje nimuhimu na Rais amekosea kufuta ama kupunguza ni hoja ya mwanasiasa muflisi .
Membe
amekua sehemu ya mfumo dhaifu ulotufikisha hapa kama Taifa,amefaidika
na safari za nje yeye binafsi bila manufaa kwa nchi,.
Membe
akumbuke kila Rais ana Vission yake .Magufuli anaamini matatizo ya
Taifa letu yatamalizwa na sisi wenyewe kwa kudhibiti matumizi ya hovyo
na yasiyoyalazima na si kwa safari za Ulaya na kuendeleza Tabia ya Kuwa Omba omba.
Ni
muhimu membe afahamu Magufuli ana style yake ,tutampima kwa matokeo as
of now hatujaona athari za safari.Membe kama yeye binafsi anatakiwa
aseme kufutwa safari kulimuathiri yeye binafsi kwa kukosa nafasi ya
Ukatibu mkuu wa Commonwealth thats why leo anakosoa.
Tunafaham maamuzi mengi ya Magufuli kwa sasa hayatafurahisha wengi walofaidika na Miradi kama NIDA Pesa za Gadafi,
walofaidika na Matumizi Mabaya ya Madaraka katika Awamu ya nne, Majipu
mengi yanayosubiri Kutumbuliwa ama yaliyotumbuliwa yatafanya jitihada
kukosoa muelekeo wa Serekali ya awamu ya Tano.
Hoja
ya kutokua na mabalozi magufuli hana siku 100 yeye amekua waziri wa
mambo ya nje for 8 yrs hakuona umuhimu wakati huo? Kuwa na balozi kwenye
nchi ni jambo Mtambuka na hasa linatazamwa zaidi kiuchumi na kisiasa .
Amekua
mmoja wa mawaziri walioua foreign relation yetu wakati wake kumekua na
malalamiko mengi juu ya mis use of funds katika wizara yake, kipindi chake Bernad Membe safari za nje walisafirishwa ma girlfirend kwa kutumia Pesa za Umma.
Nimuhimu
membe aheshimu Vission ya Magufuli na style yake inafahamika
ameathirika directly or Indirect na mchakato wa Majipu na kufunga safari
za nje.
Binafsi kama mbunge naunga mkono style ya Magufuli ya uongozi. Aliwahi kusema Sankara " You cannot carry fundamental change without a certain amount of Madness"
Mabadiliko
anayofanya sasa Ndg Magufuli yanahitaji Roho Ngumu, wendawazimu kidogo,
Kuungwa mkono na wananchi wa kawaida kwani walofaidika na udhaifu wa
awali watajitahidi kutaka kuzuia mabadiliko yoyote ambayo yanamfaidisha
aliekuwa akinyonywa hapo awali
Tutasikia watu wa aina ya Membe wengi kwakua style ya Magufuli inaathiri mfumo wao wakuwanyonya wengi na wachache kufaidika.
No comments:
Post a Comment