Bavicha Wataka Chama Cha Mapinduzi Kifutiwe Usajili Kwa Kuwa Kimeonyesha Ubaguzi wa Rangi Zanzibar
Baraza
la Viajana wa Chadema (Bavicha) limemtaka msajili wa vyama vya siasa
nchini kutoa tamko kuhusu vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyooneshwa na
baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa sherehe za
maadhimisho ya Mapinzuzi ya Zanzibar.
Akiongea
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi wa
Bavicha, Edward Simbeye alisema kuwa kutokana na vitendo hivyo vya
kibaguzi, msajili anapaswa kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria ikiwa ni
pamoja na kuifutia usajili CCM.
“Sheria
ya usajili wa vyama vya siasa iko wazi. Sheria ya usajili wa vyama vya
siasa inasema, chama chochote kitakachofanya siasa za kibaguzi huenda wa
kikabila, kidini ama vinginevyo chama hicho kitafutwa. Tunataka kauli
ya msajili wa vyama vya siasa. Ni lini, wakati gani ataifuta CCM,” alisema Simbeye.
Simbeye
alisema kuwa Baraza hilo la vijana la Chadema linamtaka msajili kutoa
tamko lake ndani ya kipindi cha siku tatu na kwamba asipofanya hivyo, watachukua hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kwenda mahakamani.
“Msajili
wa vyama vya siasa atuambie ni lini sheria hiyo imeondolewa mpaka leo
CCM ni chama cha siasa kwenye taifa hili. Vinginevyo, ndugu waandishi wa
habari tumepanga… na haya ndio maazimio ya vuguvugu hili, tutampeleka
mahakani,” alisema.
No comments:
Post a Comment