Tuesday, January 5, 2016

USIKUTE NA WEWE UMO''

USIKUTE NA WEWE UMO
Watu wengine wanashangaza sana, wanatamani sana kesho nzuri kwenye maisha tena wanapenda sana maisha matamu lakini hawako tayari kuiandaa hiyo kesho leo. Ukiwaambia wajitahidi shuleni au vyuoni basi hata sikumoja wavae kajoho ka graduu wanakuona kama wewe hamnazo, haya ukimwambia basi jiheshimu na ujitunze ili mbeleni uje upate mume au mke bora skumoja nawewe utavaa kashela au kasuti harusini wanakuona umecheleeeewa. Sasa baada ya kukosa vyote hivyo, noo sherehe ya shuleni au chuoni na noo sherehe ya harusi wala nini ndio skuhizi wanatusumbua na vimichango vya vijisherehe vya birthday kila mwaka, kisa tu mtu hana kingine cha kusheherekea isipokuwa birthday. Shuleni kapa, harusi kapa, una ya kuzaliwa tu ambayo kila kiumbe kinayo, hata yule kuku unayemla siku ya hiyo birthday yako naye mnafanana maana nayeye anahiyo siku moja tu ya kuzaliwa. Tulia ufunzwe ndugu yangu, maisha sahani ya moto - Chris Mauki

No comments:

Post a Comment