Watu Watatu Wafariki Dunia Baada ya Gari aina ya Noah Kugongana Uso kwa Uso na Basi la Adventure Mkoani Dodoma
Watu
watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya toyota Noah
yenye namba za usajili T243 DGB lililokuwa likitokea jijini Dar es
Salaam kuelekea mkoani Tabora kugongana uso kwa uso na basi la abiria la
kampuni ya Adventure lenye namba za usajili T 852 CBF lililokuwa
likitoka mkoani Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam katika kijiji cha
Buingiri madukani wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Ajali
hiyo ilitokea jana majira ya saa 9 alasiri ambapo kwa mujibu wa
mashuhuda na abiria waliokuwa ndani ya basi walisema ajali hiyo
imetokana na mwendokasi wa gari aina ya Noah ambalo dereva wake
alipoteza mwelekeo na kisha gari hilo kuhama na kulivaa basi na watu
watatu kupoteza maisha papo hapo huku mmoja akijeruhiwa vibara.
Muda
mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo jeshi la zimamoto na uokoaji
mkoani Dodoma lilifika eneo hilo na kukuta msongamano mkubwa wa magari
kutokana na ajali hiyo kuziba eneo la barabara hali iliyowalazimu
kuyaondoa magari hayo ili kuruhusu shughuli zingine kuendelea.
kwa
upande wake kamanda wa polsi mkoa wa Dodoma David Misime akizungumza
katika eneo la tukuio aliwataja miongoni mwa watu waliofariki dunia ni
dereva wa Noah aliyetambulika kwa jina la Abdalah Said Hajiru mkazi wa
Dar es Salaam huku maiti nyingine mbili zikishindwa kutambulika mara
moja ambapo pia jeshi hilo lilifanya jitihada za kuwatafutia basi
lingine abiria ili waendelee na safari yao.
No comments:
Post a Comment