Mbunge wa jimbo la ubungo ameibua
mpya tena bungeni baada ya wabunge wa chama pinzani kuondolewa na polisi nje ya
ukumbi wa bunge.
Wabunge wa chama pinzani maarufu
kama ukawa waliondolewa ndani ya ukumbi baada ya kugomea pendekezo la serikali
lililoletwa na waziri mwenye dhamana Nape
Nauye kua mikutano ya bunge isionyeshwe live na TBC na badala yake irekodiwe na
ionyeshwe usiku.
Baada ya kutoafikiana na wabunge
wa upinzani kuchachamaa mwenyekiti wa bunge Andrew Chenge aliamuru polisi kuwatoa nje
wabunge hao. Kwa mujibu wa saed kubenea
akitoa malalamiko yake bungeni alidai kua wabunge wanawake walivuliwa nguo zao za
ndani na kuvuliwa shanga zao na polisi.
No comments:
Post a Comment