Toka Bungeni : Hatimaye Bunge Latengua Kanuni Ya 94 (1)
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetengua kanuni ya 94 (1) ya
kanuni za kudumu za bunge za mwaka 2006 ili kuliwezesha bunge kujadili
mpango wa serikali utakaotaumika kwa muda wa mwaka wa fedha 2016 &
2017.
Akitengua kanuni hiyo, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu katika Serikali ya Awamu ya Tano, Jenista Mhagama
amesema kwamba bunge lilitakiwa likae kama kamati mwezi Nonemba ili
liweze kujadili mpango wa serikali lakini kutokana na uchaguzi mkuu
uliokuwepo nchini kazi hiyo ilishindikana.
Kwa
msingi huo kutokana na uwezo wa bunge kupitia ibara ya 63 (3) ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayowezesha bunge kujadili mipango
ya serikali,kwa muda muafaka serikali imeamua kutengua kanuni ili bunge
likae kama kamati kwa muda wa siku 5 ili kujadili mpango wa serikali ili
wabunge waweze kuishauri serikali kabla ya bunge la bajeti.
Aidha
mpango huo ulishindwa kujadiliwa bungeni Ijumaa iliyopita kutokana na
kanuni za bunge kukiukwa kwa kusomwa bila kutengua kanuni ya 94(1).
No comments:
Post a Comment