Majambazi Dar es Salaam Yavamia Benki Ya Access....Yaua Mlinzi na Kupora Pesa, Polisi Wapambana Nayo na Kuyaua
Majambazi
ambao idadi yao haikufahamika wakiwa na mabomu na bunduki za
kisasa jana walivamia Benki ya Access tawi la Mbagala ambako
walipora viroba vya fedha, kuua mlinzi na baadae wanne kati yao
waliuawa na jeshi la polisi.
Watu
walioshuhudia tukio hilo walisema baada ya majambazi hao
kufika katika benki hiyo kwa bodaboda nne majira ya saa nane
mchana,yalimuua mlinzi wa benki hiyo, kusha kubomoa kwa risasi
mlango wa vioo na kuingia ndani na kuzua taharuki kubwa
Mashuhuda
hao walisema, katika tukio hilo lililodumu kwa karibu saa
moja,mmoja wa majambazi hao aliyekuwa amevaa kininja,alikuwa
barabarani akiamuru magari kupita haraka huku akifyatua risasi
hovyo.
Ilielezwa
kuwa, jambazi huyo aliyeonekana kuwa na uzoefu wa matumizi ya
bunduki alikuwa akifyatua risasi kwa kutumia mkono mmoja na
ndiye aliyewajeruhi baadhi ya wapita njia.
Hivyo,wakati
uporaji ukiendelea na jambazi huyo akiimarisha ulinzi
barabarani baadae hakukuwa na magari wala pikipiki zilizokuwa
zikipita.
Mfanyabiashara
wa duka la vifaa vya ujenzi jirani na benki hiyo,Ramadhani
Tairo alisema baada ya jambazi huyo kuliona gari la polisi
likielekea eneo la tukio,alifyatua risasi na kulipiga kabla
halijafika.Gari hilo lilipoteza mwelekeo na kutumbukia mtaroni.
Tairo
alisema mbali na jambazi huyo kulipiga risasi gari la polisi
pia alilirushia bomu la mkono,lakini liliangukia barabarani bila
kuripuka.Polisi walifanikiwa kulilipua bomu hilo baadae likiwa
halijasababisha madhara kwa wananchi waliofika kushuhudia tukio
hilo.
Mkazi
mwingine wa eneo hilo,Rebecca Maliva alisema majambazi
walioingia ndani ya benki hiyo walioneka wakitoka na viroba
vitatu vya fedha ambavyo walivipakata kwenye pikipiki na kuondoka
kwa kasi kuelekea Mkuranga kupitia barabara ya Kilwa.
Rebecca
alisema polisi zaidi walifika kwenye eneo hilo wengine wakiwa
kwenye pikipiki na kuanza kuwafukuza majambazi hao ambapo
walipofika eneo la shule ya St. Marry's,walitupa kiroba kimoja
cha fedha ambacho wananchi waliokuwa jirani waligombania na
kuchukua fedha zilizokuwemo na kisha kila mmoja kukimbia na
burungutu la noti.
Baada
ya nusu saa wakati umati ukiwa bado upo kwenye benki
hiyo,magari ya polisi yalipita katika eneo hilo yakitokea eneo
la Mkuranga yakiwa yamebeba miili ya majambazi yaliyouawa.
Magari hayo yalikuwa yakisindikizwa na vijana wa bodaboda waliokuwa wakishangilia kazi iliyofanywa na polisi.
Kamanda
wa p[olisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro
alizungumzia kwa ufupi tukio hilo n kwamba majambazi manne
yaliuawa na kukamata silaha tatu,lakini hakutaka kuingia kwa
ndani akisema atatoa taarifa zaidi leo
No comments:
Post a Comment