Bungeni: Serikali Kuajiri Vijana 71,408 Mwaka Huu.......Halmashauri Zaagizwa Kutenga Asilimia 5 Ya Mapato Kwa Ajili Ya Kuwasaidia Vijana
Serikali
katika mwaka wa fedha 2016/2017 imepanga kuongeza ajira kwa vijana ili
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wa
kitanzania kwa kuongeza ajira na kuwezesha wengine kujiajiri kupitia
mifuko ya uwezeshaji toka Halmashauri za Wilaya nchini.
Akijibu
swali la Mhe.Mgumba Tebweta Omary Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM) lenye
sehemu a na b lililouliza Serikali itaanza lini kuwawezesha vijana wa
Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki kifedha ili waweze kujiajiri na
kuondokana na tatizo la ajira na umaskini ,Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe Suleiman Jafo
amesema vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kusini Mashariki
wamekuwa wakiwezeshwa kiuchumi kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana ambapo kila Halmashauri hupaswa kutenga asilimia 5 ya mapato yake
ya ndani kila mwaka kwa ajili ya vijana.
Mhe
Suleiman Jafo ameongeza kuwa katika Bajeti ya mwaka
2014/2015,Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilifanikiwa kutoa Shillingi
Millioni 10.3 kwa vikundi vya vijana 19 kwa ajili ya kutekeleza shughuli
mbalimbali za kiuchumi na katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016
vikundi vya vijana vilitengewa Shilllingi Millioni 87.5 ili kuviwezesha
kiuchumi kwa kujiajiri.
“Katika
kutatua changamoto zilizopo kwa vijana tunawawezesha kifedha ili
kujiajiri ili kumekuwa na tatizo la fedha kuchelewa kufika kwa walengwa
ila Serikali kupitia Wizara yangu tunalifanyia kazi ili fedha zifike kwa
wakati na tumetenga Shillingi Millioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya
kuwezesha vijana walioko katika vikundi mbalimbali mfano SACCOS ili
waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi kwa kujiondoa katika hali ya
umaskini”
“Napenda
kuwaomba wabunge tusaidiane sababu wao wanahusika katika kamati za
fedha za Halmashauri za Wilaya, waende wakasimamie hizo fedha kwa ajili
ya kuwezesha vijana zitoke na ziwasaidie walengwa” Alisema Mhe Jafo.
Aidha
Mhe Suleiman Jafo amesema kuwa Serikali imetenga Shillingi Billioni
233 kwa ajiri ya kuajiri vijana wapya takribani 71,408 kati ya hao
watumishi wapya wa Afya wanatarajiwa kuwa takribani 10,871 na Waalimu
40,000 kwa nchi nzima ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana
wanaomaliza vyuo mbalimbali nchini.
Serikali
kupitia Halmashauri za Wilaya imejipanga katika kuwawezesha vijana
katika maeneo yao kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri na kwa mwaka wa
fedha 2016/2017 Serikali itaboresha zaidi mifuko ya kuwezesha vijana
katika Halmashauri za Wilaya kwa kununua vifaa zaidi vya kujifunza stadi
mbalimbali za kazi zitakazowezesha vijana wengi zaidi kuwa na ujuzi
utakaowasaidia kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment