Majipu Yaendelea Kutumbuliwa......Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Asimamishwa Kazi
WAZIRI wa nchi,ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora,Angella Kairuki amemsimisha kazi mkuu wa chuo cha utumishi wa umma nchini Said Nassoro kutoka na uzembe ulioisababishia serikali hasara ya bilioni 1.
Vilevile Waziri Kairuki amewasimamisha kazi Mkuu wa chuo hicho tawi la Dar es salaam,Joseph Mbwilo na Silvanus Ngata ambaye naye ni Mkuu wa chuo hicho tawi la Tabora.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Waziri Kairuki amesema amefikia hatua hiyo ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada ya kubaini utendaji usioridhisha katika vyuo hivyo.
Amesema Nassoro amemsimisha kazi baada ya kushindwa kuwasimamia watumishi wa chini yake katika chuo hicho.
“Mwaka 2011 hadi 2013 bwana Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi wa jengo la chuo hicho tawi la Mtwara tofauti na fedha iliyokuwa imepangwa.
"Chakushangaza, huyu Nassoro ambaye ni mkuu wao, baada ya kugundua kosa hilo alishindwa kumuwajibisha na badala yake aliamua kumhamishia tawi la chuo cha Tabora. Sasa mimi nawasimamisha kazi wote ."Amesema Kairuki
"Chakushangaza, huyu Nassoro ambaye ni mkuu wao, baada ya kugundua kosa hilo alishindwa kumuwajibisha na badala yake aliamua kumhamishia tawi la chuo cha Tabora. Sasa mimi nawasimamisha kazi wote ."Amesema Kairuki
Pia waziri Kairuki amesema amemsimamisha Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za chuo.
“Huyu Mbwiro kwa mwaka 2013 alitumia vibaya fedha za ada za wanafunzi kiasi cha bilioni 1 ,lakini licha ya ubadhilifu huo, Nassoro alimteua bwana Mbwiro kuwa Kaimu mkuu wa chuo kwa upande wa fedha." Alisema Waziri Kairuki.
Wakati Waziri Kairuki akitumbua majipu hayo,mmoja wa watendaji hao,Said Nassoro alikuwepo kwenye mkutano huo na wanahabari huku akiwa hajui kinatakachotokea
No comments:
Post a Comment