John Woka ni msanii ambaye Tanzania ilikuwa nae sana kwenye chati za
muziki wa bongofleva kupitia kundi la Watukutu,
na sasa Tanzania imepata taarifa za kifo chake kilichotokea alfajiri
ya February 16 ikiwa ni saa kadhaa tu baada ya kupelekwa
Hospitali.
Woka amefariki baada ya kupata ajali wakati anatengeneza
gari Sinza kwenye mfumo wa AC inasemekana
kuna kitu kilifyetuka baada ya kufungua AC na kumpiga
kwenye paji la uso na kuingia kama inchi 3 au 2 hivyo damu nyingi zikaanza
kumtoka kichwani na mpaka anafikishwa hospitali, Woka alikuwa
katika chumba cha wagonjwa Mahututi.
Kifo cha John Woka ni
pengo jingine kwenye bongofleva, alipita kwenye chati mbalimbali za muziki huu
kutokana na nyimbo zake kama mganga na hii kitu hii
ambazo alizipiga kwa kurap kama mlevi.
No comments:
Post a Comment