Wadaiwa Sugu Bodi ya Mikopo Kitanzini......CAG Apewa Jukumu La Kuwasaka Popote Walipo,Kutoajiriwa Sio Kigezo Cha Kukwepa Deni
BODI
ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetoa onyo kwa wadaiwa sugu ambao
hawajajitokeza kuanza kulipa madeni yao, kwamba hatua mbalimbali dhidi
yao zinatafuata kokote waliko.
Miongoni
mwa hatua hizo, bodi hiyo imetaja kuwa ni kuwatoza wadaiwa hao sugu
riba ya asilimia kumi katika deni lao na kutumia taarifa zao kuwazuia
kufanya safari za nje ya nchi.
Taarifa
ya hivi karibuni ya bodi hiyo , imeeleza kuwa wadaiwa hao wa tangu
mwaka wa masomo wa 1994/95, wataanza kusakwa kupitia Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye anawajibika kukagua mali zote
za Serikali.
Mbali
na CAG, ambaye ana mkono mrefu wa kuwasaka katika ofisi zote za
Serikali Kuu, Mashirika ya Umma, Serikali za Mitaa na katika miradi
ambayo Serikali ina ubia na sekta binafsi, pia kampuni binafsi za
ukaguzi wa hesabu, zenye mkono mrefu katika sekta binafsi, zitatumika
kuwasaka katika kampuni binafsi na asasi za kiraia.
“Jukumu
la CAG na kampuni zingine binafsi za ukaguzi wa mahesabu, ni
kulazimisha waajiri kuwasilisha taarifa za wafanyakazi wao ambao ni
wahitimu wa elimu ya juu na makato ya mkopo waliopewa,” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa
hiyo imefanya marejeo ya Sheria ya Bodi namba 9 ya 2004 na marekebisho
yake, inayomtaka kila mwajiri kutoa maelezo kwa maandishi kwa bodi,
kuhusu mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo huo, ndani ya siku 28 tangu
mdaiwa alipoajiriwa.
Hatua
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, mdaiwa yeyote wa bodi hiyo atakayeshindwa
kulipa deni lake bila sababu za msingi, kwanza atakuwa akikabiliwa na
kesi ya madai chini ya kifungu cha 6 C na H cha Sheria ya Bodi ya Mikopo
namba 9 ya mwaka 2004.
Mbali
na kukabiliwa na kesi hiyo, pia mkopo wake kwa namna unavyochelewa
kuanza kulipwa, utakuwa ukijilimbikizia riba ya asilimia 10.
Taarifa
hiyo ya bodi imeeleza kuwa mdaiwa huyo taarifa zake zitapelekwa katika
taasisi za kumbukumbu ya mikopo zilizo chini ya Benki Kuu (BoT), ambazo
zitazuia wadaiwa hao kupata mikopo katika mabenki na asasi zote za
fedha.
Mdaiwa
huyo pia atazuiwa kupata udhamini wa Serikali katika muendelezo wa
masomo yake, lakini pia atazuiwa kujiunga na chuo chochote cha elimu ya
juu ndani na nje ya nchi.
Aidha
kwa mujibu wa taarifa hiyo, taarifa zao pia zitawasilishwa katika Idara
ya Uhamiaji iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na katika
ofisi zote za kibalozi, ili wakose kibali cha kusafiri nje ya nchi.
Hasara
nyingine watakayokabiliwa nayo wadaiwa hao, ni Tozo ya Kulinda Thamani
ya Mkopo (VRF) ya asilimia sita kila mwaka, itakayotozwa kwa kila mkopo,
ili wadaiwa watakapoanza kulipa mkopo waliochukua, walipe kwa thamani
ya sasa.
Tozo
hiyo imelenga kuepuka athari ya mfumuko wa bei tangu mdaiwa
aliponufaika, lakini pia kuwezesha urejeshwaji wa deni, uwe na thamani
ya kumhudumia mwanafunzi mwingine mwenye mahitaji kwa sasa na baadaye.
Ambao hawajaajiriwa
Taarifa
hiyo pia imeonya wadaiwa wanaodhani kuwa kutokuajiriwa ni sababu ya
kutolipa mkopo huo, kwamba mkopo huo unatakiwa kulipwa baada ya
kumalizika kwa mwaka mmoja tangu mdaiwa alipofanikiwa kuhitimu masomo
yake, au mwaka mmoja tangu mhusika alipokatisha masomo yake kwa sababu
yoyote.
Aidha,
taarifa hiyo imeelekeza watakaojitokeza, kama wameajiriwa, asilimia
nane ya mshahara wao wa kila mwezi, itatakiwa kukatwa na kuwasilishwa
kwenye Bodi ili kulipa deni husika.
Lakini
pia Bodi hiyo imetengeneza utaratibu kwa ambao hawajaajiriwa, kwamba
wanaweza kulipa kiasi cha chini cha Sh laki moja kila mwezi katika
akaunti za Bodi zilizopo Benki ya Posta yenye namba CCA0240000032; Benki
ya NMB namba 2011100205 na Benki ya CRDB namba 01J1028467503.
Deni lenyewe
Kwa
mujibu wa Ripoti ya CAG, hadi Juni 2014, bodi hiyo ilikuwa imewakopesha
wanafunzi Sh trilioni 1.8 kuanzia mwaka wa masomo 1994/95 na kati ya
fedha hizo, Sh bilioni 51 zilitolewa na iliyokuwa Wizara ya Elimu ya
Juu, Sayansi na Teknolojia.
Taarifa
hiyo ya HESLB imetolewa siku chache kabla ya Waziri wa Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kusitisha ajira ya
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, George Nyatega kwa tuhuma za udhaifu
katika fedha za mikopo zaidi ya Sh bilioni 3.2.
No comments:
Post a Comment