Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepongeza Chama cha National Resistance
Movement (NRM) cha nchini Uganda kwa ushindi katika Uchaguzi Mkuu
uliofanyika Februari 18.
Kutokana na ushindi huo CCM inampongeza Rais mteule, Yoweri Museveni ambaye ndiye mwenyekiti wa NRM.
Taarifa
iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa CCM, Daniel
Chongolo imeeleza kuwa wamefuatilia kwa ukaribu mchakato wa uchaguzi huo
na walikuwa na imani kwamba NRM itaibuka mshindi dhidi ya waliokuwa
wagombea wengine saba wa urais.
=====
No comments:
Post a Comment