Bungeni: Serikali Kuimarisha Miundombinu Kuboresha Utalii Nchini.
Serikali
imejipanga kuimarisha miundombinu inayoelekea kwenye mbuga za wanyama
na vituo vingine vya utalii nchini ili kuboresha utalii wa ndani na wa
nje ya nchi kwa kujenga barabara ili kuwezesha watalii kufika kwa
urahisi katika sehemu za vivutio vya kiutalii.
Akijibu
swali la Mhe.Risala Said Kabongo Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA)
lililouliza serikali ina mikakati gani kuboresha miundombinu ya
barabara, malazi na viwanja vya ndege katika hifadhi, Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani amesema jitihada zimefanya na
zinaendelea kufanywa ili kuboresha na kuimarisha barabara mbalimbali
zinazoelekea katika hifadhi mbalimbali nchini kwa kiwango cha lami ili
kuongeza wigo wa watalii kutembelea maeneo hayo kwa urahisi.
Amezitaja
barabara ambazo zilizoko kwenye mpango wa kuziboreshwa ili kurahisisha
watalii kuyafikia maeneo hayo kuwa ni barabara ya Sumbawanga-kasanga,
barabara ya Kigoma kuelekea kusini hadi Kalya na Mwese.
“Sio
tutaboresha barabara tu ila tunaviangalia pia viwanja vya ndege
vinavyotumika kwa kuviimarisha na kuviboresha viwanja vya ndege vya
Songwe,Kigoma na Mpanda ambavyo vitasaidia kufikika kwa urahisi maeneo
ya vivutiio
“
Tunaendelea kuvutia wawekezaji binafsi kutoa huduma mbalimbali za
watalii kama malazi na mpka sasa tumetoa vibali 11 kwa wawekezaji
kuwekeza katika malazi yaani Hoteli za kitalii katika Hifadhi za
Ruaha,Mikumi,katavi na Mahale na uwekezaji huo uko katika hatua za
utekelezaji” Alisema Mhe. Ramo Makani.
Wizara
kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na
Shirika la USAID inaandaa mikakati ya kuendeleza na kuutangaza utalii
kwenye maeneo mbalimbali na kuboresha miundombimu ili kuwezesha watalii
kufikia vivutio kiurahisi.
No comments:
Post a Comment