Mtumishi
wa nyumbani mwenye umri wa miaka 23, aliyekuwa akifanyakazi katika
nyumba iliyo eneo la Mwika-Mrimbo, Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro,
amekufa kwa madai ya kulawitiwa na bosi wake, Zablon Shaaban (32).
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, William Nyello jana alithibitisha
akisema tukio hilo ni la Januari 25, mwaka huu saa 3 usiku katika kata
hiyo.
Alisema
mtumishi huyo wa nyumbani alifanyiwa kitendo hicho na bosi wake
aliyekuwa akiishi naye baada ya kurejea nyumbani wakitokea matembezini
jioni.
“Mtuhumiwa
alikuwa akiishi na marehemu nyumba moja, waliporejea katika matembezi
ya jioni na wakati wa kulala, mtuhumiwa alimfuata marehemu chumbani
kwake na kumkaba koo na kumlawiti,” alisema Nyello.
Kaimu
Kamanda alisema kutokana na kitendo hicho, kilichothibitishwa pia kwa
uchunguzi wa daktari, polisi inamshikilia mtuhumiwa huyo na atafikishwa
mahakamani.
No comments:
Post a Comment