Chadema Waungana na ACT -Wazalendo........Wadai Serikali ya Magufuli ni ya kidikteta
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekosa imani na serikali ya
awamu ya tano kwa kuwa na matendo ya kidikteta na kwenda kinyume na
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kwa kuminya uhuru wa
wananchi wa kupata habari.
Hayo
yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam, na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema,
Salum Mwalimu alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ambapo amesema
kuwa serikali imekuwa ikijinadi kwa kauli mbiu ya hapa kazi huku ikiwa
mstari wa mbele kwa kuwanyima haki ya msingi wananchi ya kupata habari.
Amesema
kuwa matendo hayo ni pamoja na kuzuia Shirikia la Utangazaji la
Tanzania(TBC), kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mikutano ya bunge
inayoendelea ,kufutwa kwa Gazeti la Mawio pasi na sababu za
msingi,kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara, na kuunda
kamati dhaifu bungeni.
Amesema
kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye ametoa
sababu zisizokuwa za msingi ambapo alidai kuwa serikali inaepuka gharama
za kurusha matangazo hayo moja kwa moja na baadala yake kurekodi vikao
hivyo vya bunge kwa kurushwa saa nne usiku.
Amesema
inaonekana Waziri huyo hajafanya utafiti na kwamba ikiwa tatizo lipo
kwenye gharama alizotaja chadema ipo tayari kuchangia gharama hizo kwa
kuanzisha harambee maalumu pamoja kuwataka chama cha wamiliki wa vyombo
vya Habari (Moat) na Baraza la Vyombo vya Habari (MCT) kulisimamia suala
hilo.
“Nape
ataje gharama hizo tutachangishana ......mwenye mia moja mia mbili ili
wananchi wajue mambo muhimu yanayoendela kwa wakilishi wake”,amesema Mwalimu.
Amesema
Nape alikuwa anayumba kwa kuwa na ndimi mbili kwa kuongeza sababu
nyingine ya kuzuia kurusha kwa matangazo hayo ni kuwa muda huo ni wa
kazi na kwamba watu watakuwa hawafanyi kazi kutokana na kuangalia bunge.
Amesema
kuwa hoja ya watu kutofanya kazi haina mashiko kutokana na watu huwa
wanafanya kazi ilhali bunge linaendelea ambapo kama kuna hoja muhimu
watu huzisikia bila kuathiri shuguli zao lakini kuna wengine muda huo
sio wa kazi kwao.
Amesema kuwa serikali imekusudia kuminya uhuru wa habari kutokana na matukio yaliyofuatana ya kushugulikia vyombo vya habari.
Amesema
kuwa serikali imezuia mikutano ya siasa ambapo Waziri Mkuu Kasimu
Majaliwa na Nape Mnauye walitoa kauli hizo walipokuwa Mkoani Lindi na
baadaye Jeshi la Polisi kuweka mkazo wa suala hilo.
Amesema
suala hilo hawawezi kulikubali kutokana na chama kuwa na mikutano yao
kila baada ya muda na kwamba muda wa kuratibu mikutano hiyo watafanya
vikao vyao.
Amesema
serikali imeunda kamati dhaifu bungeni kwa nia ya kudhoofisha shughuli
za utendaji bungeni na maendeleo ya nchi kwa kuwaweka wabunge wageni
kwenye kamati muhimu ilhali hawana uwezo kuzisimamia ambapo kamati
ambazo hazina umuhimu kupangiwa watu wenye uwezo.
No comments:
Post a Comment