Monday, January 11, 2016

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akutana na Mbwana Samatta Dar na Kumpongeza kwa Kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametembelewa ofisini kwake na mwanasoka bora Afrika kwa wachezaji wa ndani Mbwana Samata leo asubuhi  na kufanya nae mazungumzo ikiwa ni sehemu ya kumpongeza kwa mafanikio hayo makubwa ambayo Mbwana ameyapata na heshima kubwa aliyoiletea Taifa kwa ujumla.

Baada ya mazungumzo hayo Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete, Mbwana Samata pamoja na Muenezi wa CCM ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye walikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia mafanikio ya Samata na kusema wao kama Chama tawala wamepokea  ushindi wake kwa furaha kubwa

No comments:

Post a Comment