Sunday, January 17, 2016

TCRA YAVIFUNGIA VITUO VYA RADIO NA TV


 Image result for TCRA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Ally Simba
Adhabu hiyo iliyotokana na vituo hivyo kushindwa kulipia ada ya leseni, inaanza rasmi Jumatatu, January 18.
Vituo vya Sahara Media Group ndivyo vilivyoathirika zaidi. Vituo vya redio, Radio Free Africa na Kiss FM pamoja na kituo cha runinga cha Star TV vilivyo chini ya kampuni hiyo vyote vimefungiwa.
TCRA imedai kufikia hatua hiyo, baada ya vituo hivyo kukiuka sheria ya Utangazaji na Posta ya Mwaka 2014 ambayo inavitaka vituo hivyo kulipia ada ya leseni ya matangazo kwa kila mwaka na ada ya masafa.
“Kifungu cha 22 cha sheria ya EPOKA ambayo ipo sura 306 na kifungu cha 21(g) inasema kuwa kampuni inaposhindwa kulipia ada ya reseni inapewa siku 30 ili aweze kulipa lakini hawa tumewapa taarifa lakini wamekaidi na wengine wanadaiwa tangu mwaka jana,kwahiyo sheria inasema wazi na sisi tumewapa notice ya siku 30 na bado wakawa wanasuasua kulipa, tumevifungia kwa miezi mitatu” Afisa Habari wa mamlaka hiyo, Innocent Mungi aliiambia blog ya Full Habari.
Vituo hivyo vinatakiwa kuzima matangazo yake kuanzia usiku wa Jumapili, Jan 17. Habari njema ni kuwa kituo kitakacholipa deni lake ndani ya miezi hiyo mitatu kitaruhusiwa kurudi hewani.
“Katika kipindi cha miezi mitatu kituo chochote kikilipa ada ya lesini ,na akatimiza matakwa yote ya kisheria na akalipa pesa zote anazodaiwa basi sisi tutamfungulia,” alisema Mungi na kusisitiza kuwa kama kituo kitashindwa kulipa ada hiyo ndani ya kipindi hicho kitanyang’anywa kabisa leseni.
HIVI NI VITUO VILIVYOFUNGIWA
1. Sibuka FM
2. Breez FM
3. Country FM
4. Ebony FM
5. Hot FM
6. Impact FM
7. Iringa Municipal TV
8. Kiss FM
9. Kitulo FM
10. Kifimbo FM
11. Mbeya City Municipal TV
12. Radio 5
13. Radio Free Afrika (RFA)
14. Musa Television Network
15. Pride FM radio
16. Radio Huruma
17. Radio Uhuru
18. Star TV
19. Rock FM Radio
20. Standard FM radio
21. Sumbawanga Municipal TV
22. Tanga City TV
23. Top Radio FM limited
24. Ulanga FM

No comments:

Post a Comment