JUMUIA
ya Wanazuoni Watetezi wa Rasilimali nchini (JUWARA), imewataka wabunge
wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajia kuanza rasmi
vikao vyake vya kujadili hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa kulizindua
bunge hilo hapo kesho,
kumuomba na kumkumbusha Rais DK. John Pombe Magufuli kutoa agizo la kukamatwa mara moja kwa mfanyabiashara Harbinder Sing Sethi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya IPTL/PAP inayoendesha mtambo wa kufua umeme wa dharura uliopo tegeta Salasala kama sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge lililopita .
kumuomba na kumkumbusha Rais DK. John Pombe Magufuli kutoa agizo la kukamatwa mara moja kwa mfanyabiashara Harbinder Sing Sethi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya IPTL/PAP inayoendesha mtambo wa kufua umeme wa dharura uliopo tegeta Salasala kama sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge lililopita .
Wanazuoni
hao wamesema kuna kila sababu ya wabunge wa bunge hili la 11 kusimama
imara ili kutetea rasilimali za taifa letu zinazoonekana kutafunwa na
wajanja wachache wanaotumia visingizio dhaifu vya sheria na uwekezaji
kwa kumtaka Rais John Magufuli aharakishe utekelezwaji wa maazimio hayo
ya Bunge hasa azimio namba moja lililoitaka serikali kumchukulia hatua
kali na kumkamata mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Herbinder Sing Seth kwa
makosa ya kulisababishia taifa hasara ya zaidi ya bilioni 320 kutokana
na wizi uliofanyika katika akaunti ya TEGETA ESCROW.
Pia,
jumuia hiyo imesema ina imani kubwa na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo huku ikimtaka awe mwangalifu na asiwe mtetezi
wa IPTL safari hii kwa kuwa maamuzi ya bunge yalikuwa sahihi dhidi ya
kampuni hiyo, ambayo imeisababishia hasara kubwa serikali kutokana na
vitendo vyake vilivyofanya.
Wakizungumza
na JAMVI LA HABARI, Mwenyekiti na Katibu wa Jumuia hiyo, Omary Kisambu
na Mahmud Salibaba kila mmoja,wameonyesha kusikitishwa na kitendo cha
serikali kumkumbatia mfanyabiashara huyo, anayelalamikiwa na watanzania
wengi kwa kulitia hasara taifa kutokana na vitendo vyake alivyovifanya
kwenye sakata nzima la akaunti ya Tegeta Escrow.
"Tunashangaa
mpaka sasa mapendekezo na maazimio muhimu ya Bunge kuhusu TEGETA ESCROW
hayajatekelezwa na badala yake wameishia kuwatoa kafala kina William
Ngeleja na Anna Tibaijuka, hii haitakiwi kuachwa ipite hivi hivi, lazima
kama vijana wasomi tusimame kidete kupigania taifa letu na rasilimali
zake" alisema Mwenyekiti huyo.
Naye,
Katibu wa Elimu na Mawasiliano wa Jumuia hiyo, Mahmud Salibaba
amelinukuu azimio namba moja na kushangaa kuona serikali imekubali
kutekeleza azimio namba nane wakaliacha azimio namba moja ambalo
linahitaji utekelezaji tu.
Mahmud aliongeza kuwa azimio namba moja linasema
"Bwana
Harbinder Singh Seth na wengine,Bunge linaazimia kwamba, TAKUKURU,
Jeshi la Polisi na Vyombo vingine husika vya Ulinzi na Usalama, vichukue
hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, dhidi ya watu wote
waliotajwa na Taarifa Maalumu ya Kamati, kuhusika na vitendo vyote vya
kijinai kuhusiana na Miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine
watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea kuhusika
katika vitendo vya jinai". Aliinukuu.
Katibu huyo, alisema "Hatuna
wasiwasi na Prof. muhongo, Tunaamini ana mapenzi mema na utayari wa
kulitumikia taifa katika sekta hii, lakini kwenye hili tunamtaka aweke
mbele maslahi ya Taifa na kamwe asigeuke kuwa mtetezi wa IPTL wala
Sethi".
Wanazuoni
hao wameendelea kuonyesha matumaini yao kwa Bunge hili huku wakiamini
kwamba kama ilivyo kawaida ya mabunge yaliyotangulia, panapotokea
masuala ya kitaifa yenye maslahi mapana kwa nchi basi wabunge wav yama
vyote huungana na kuweka tofauti zao pembeni na kulisimamia taifa liokoe
rasilimali zake.
IPTL/PAP YAMZUIA ZITTO KABWE KUZUNGUMZIA.
Wakati
hayo yakiendelea, kampuni hiyo inayolalamikiwa kuingizia hasara ya
mabilioni serikali na kupelekea kuwajibishwa kwa watumishi kadhaa wa
umma, imejitokeza na kuwataka wabunge waache kulizungumzia suala hilo
kwa kuwa bado lipo mahakamani.
Katika
taarifa iliyosambazwa kama tangazo iliyosainiwa na Katibu na Mshauri
mkuu wa sheria wa Kampuni hiyo, Joseph Makandege, imemtaka Mbunge wa
Kigoma Mjini, Zitto kutokuendelea kulizungumzia suala hilo na kwamba
aache mpango wake wa kutaka kulifufua upya suala hilo hasa bungeni kwa
kuwa tayari kampuni hiyo imeshamshitaki katika kesi ya madai iliyopo
mahakama kuu na kwamba haitakuwa busara kwa mbunge huyo kulizungumzia
suala hilo ambalo yeye binafsi ana maslahi nalo.
Kadhalika
taarifa hiyo inasema kwamba tayari serikali imejibu kupitia hotuba ya
Rais mstaafu Jakaya kikwete pindi alipokuwa madarakani kuwa haipo tayari
kumkamata Sethi wala kutaifisha mitambo hiyo kwa kuwa itasababisha
kuanzishwa kwa mahusiano mabovu na wawekezaji, hivyo Makandege
amesisitiza kwamba ni vema mbunge huyo na mbunge mwingine yoyote aachane
na mpango wa kuliibua suala hilo bungeni.
‘’kwa
uelewa wetu mdogo kuhusu maswala haya, kauli ya Rais huwa ndio kauli ya
mwisho na ni sawa na hukumu, na tayari Rais (Rais Mstaafu Kikwete)
alishasema kuwa suala hilo haliwezekani ‘’. Ilisisitiza taarifa hiyo ya Makandege.
‘’katika
hali ya kiubinaadamu, si vema kwenda bungeni kushusha lawana na tuhuma
kuwatuhumu watu na ama kampuni ambazo zenyewe haziwezi kuingia bungeni
kujitetea’’. Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
‘’Hata
mheshimiwa Zitto alifanya makosa kujihusisha na suala la IPTL/PAP
wakati akijua kuwa ameshtakiwa mahakamani na kwamba moja kwa moja
anakuwa na mgogoro wa kimaslahi, japo hajatamka mahala popote kuwa ana
mgogoro wa kimaslahi na sakata husika’’. Iliongeza sehemu ya taarifa hiyo
ZITTO KABWE AWAJIBU .
Naye
mbunge wa Kigoma mjini ACT – WAZALENDO ambaye wakati wa mjadala wa
sakata hilo la ESCROW alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayosimamia
hesabu za serikali, amejibu taarifa hiyo kwa kusema ni ya uongo
inayoambatana na uoga wa kuwajibishwa na bunge baada ya kugundua maovu
yao na kwamba IPTL /PAP hawana mamlaka ya kisheria kumzuia mbunge
kujadili swala lolote ndani ya bunge akiwa anatimiza wajibu wake wa
kikatiba.
‘’Sikuwa
na soma ripoti yangu wala kuwasilisha maoni yangu, nilikuwa nawasilisha
ripoti ya kamati ya kudumu ya bunge kwa hiyo si sahihi kulihusisha
swala lile na mambo binafsi’’inasema taarifa ya Zitto Kabwe
‘’Mpaka
wakati nawasilisha taarifa ya kamati bungeni, sikuwa nimewahi kupokea
hicho wanachosema ni shitaka lao kwangu, kwa kuwa tumesoma ripoti mwezi
November mwaka 2014 na nimeletewa shitaka lao mwezi mei mwaka 2015, kwa
hiyo sikuwa na mgogoro wowote wa kimaslahi kama wanavyotaka kuuaminisha
umma’’. Iliongeza taarifa ya mbunge huyo.
Zitto
aliongeza zaidi kwa kusema kwamba mpaka sasa hajapokea taarifa ya
kimahakama ikimzuia kutokujadili hoja inayohusiana na yeye kujadili
jambo linahusiana na IPTL/PAP na badala yake amepokea taarifa ya kesi ya
madai ya fedha na hivyo haki zake za kutumia katiba kujadili maswala ya
kitaifa ndani ya bunge zipo pale pale na kwamba ataendelea
kuwawakilisha watanzania kwa kusimamia rasilimali za taifa.
Sakata
la IPTL na akaunti ya ESCROW lilibua hisia mbali mbali wakati wa
mjadala wake uliodumu kwa zaidi ya miezi saba mwaka juzi na kuhitimishwa
mapema January mwaka jana baada ya Waziri Muhongo kujiuzulu
Credit: Jamvi La Habari
No comments:
Post a Comment