Sunday, January 17, 2016

STAR TV YATOA TAMKO HILI BAADA YA KUFUNGIWA


Manejimenti ya sahara media group ambao ni wamiliki wa Star Tv, RFA na Kiss Fm  imesema haijapata barua au taarifa rasmi yeyote kutoka mamlaka ya mawasilano Tanzania TCRA  ya kutakiwa kufunga vyombo vyake

Imesema wameshtushwa na taarifa hiyo ikizingatiwa kwamba wamekuwa wakilipia leseni ada zake na ada za masafa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 500 hadi kufikia mwezi October 2015.

Wamesema yamekuwapo mawasiliano ya mara kwa mara kati ya TCRA kanda ya Mwanza, makao makuu na sahara media group limited nakukubaliana juu ya utaratibu wa malipo ya ada husika.

Lakini menejimenti imeshangazwa na hatua hiyo ya TCRA kutangaza kuvifungia vituo vyake kupitia mkutano wa  vyombo vya habari bila kujali athari zakufungia vyombo vya kitaifa kwa walaji na watoa huduma.

Sahara media group limited imekuwa ikilalamikia utozwaji wa ada kwa dola za kimarekani jambo ambalo limekuwa likipandisha ada hizo kila mara na kufanya ulipwaji wa ada hizo kibajeti kukwama kwama.

Menejimenti pia imelaani taarifa hiyo kutolewa mwishoni wa wiki nakuvipa vituo husika siku mbili tu kukamilisha ulipaji ada wakijua dhahiri jumamosi na jumapili sio siku za kazi.

Menejimenti ya star tv  inawaondoa wasiwasi watazamaji na wasikilizaji wake,  hatua  thabiti zitachukuliwa ili kumaliza tatizo hili kwa sahara media group limited  na TCRA Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria, Kanuni Na Maridhiano.

No comments:

Post a Comment