Rais Magufuli Awaapisha Balozi Na Makatibu Tawala Wawili.....Amtuea Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mnadhimu Mkuu JWTZ
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
30 Januari, 2016 amewaapisha Balozi, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi
Tanzania na Makatibu Tawala wawili, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Walioapishwa ni:
Balozi Mahadhi Juma Maalim, ambaye anakuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Kuwait.
Luteni
Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, ambaye anakuwa Mnadhimu Mkuu wa
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akijaza nafasi iliyoachwa wazi na
Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba, ambaye amestaafu. Kabla ya Uteuzi
huu Luteni Jenerali Mabeyo alikuwa Mkuu wa Usalama na Utambuzi wa Jeshi
la wananchi Tanzania.
Kamishna
Paul Moses Chagonja, ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi,
akijaza nafasi iliyoachwa wazi Madeni Kipande ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Kamishna
Clodwig Mathew Mtweve, ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,
akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Akizungumza
baada ya kuapishwa, Balozi Mpya wa Tanzania nchini Kuwait Mheshimiwa
Mahadhi Juma Maalim, ameahidi kuiwakilisha vyema Tanzania nchini Kuwait
hususani katika uchumi ili Tanzania iweze kunufaika na ushirikiano
uliopo baina ya mataifa haya mawili.
Nae
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi wa wananchi Tanzania Luteni Jenerali Venance
Salvatory Mabeyo, ameahidi kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na
Mtangulizi wake Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Albert Ndomba ya
kuhakikisha anamshauri vizuri Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na hivyo
kuliwezesha Jeshi hilo kutekeleza wajibu wake ipasavyo.
Kwa
upande wao, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna Clodwig Mathew
Mtweve na Katibu wa Mkoa wa Katavi Kamishna Paul Moses Chagonja,
wameahidi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa katika kusukuma gurudumu la
maendeleo kwenye mikoa waliyopangiwa, ikiwemo kusimamia nidhamu kwa
watumishi wa umma.
Gerson Msigwa,
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
30 Januari, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania Ikulu
jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akimuapisha Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kuwa Mnadhimu
Mkuu wa JWTZ Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve kuwa Katibu Tawala
wa Mkoa wa Mwanza Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
No comments:
Post a Comment