Friday, January 8, 2016

presha yapanda na kushuka(shairi)




Presha ya panda na kushuka.moyo wa dunda kama  wataka pasuka
Sina amani usiku na weweseka,ee moyo wangu kwann umetekeka
Sasa waona madhara ninayoyapata, sina usemi nateseka mateka,
Umenipendesha nisiko pendeka,mawazo yasafiri pilika pilika,
Nabaki naumia afya yadhoofika,sijaitwa ila naitika,
Ee mola ninusuru na haya madhira yaliyonifika


Maelezo tosha nakosa,
Kueleza yalonifika,
Wenye uchungu mkasa,
Mtima wangu mateka,
Maumivu nasahau falsafa,

Naulaumu wangu moyo,
Mahaba yanipa chongo,
Nachukia yake choyo,
Iloninyima mchongo,
Naonekana poyoyo,

Natapa nikitafuta,
Msaada wapi nipate,
Kwa haya yalonipata,
Shujaa gani nimfuate,
Dira yake kuifuata,
Jasho chozi navuja,
Maumivu tele pomoni,
Hata jinale nikitaja,
Kisu chapenya moyoni,
Kupenda tena si haja,

tosha kwangu fundisho,
darasa limenitosha,
maumivu sasa mwisho,
maishani nayakatisha,
akili naifumbua iona  kesho,



Kwenye moyo yamekita
Ninaye mpenda,hanitaki  kata
Hasikii hata nikibembeleza
Adai mapenzi na mimi hapana labda rafiki au kaka
Moyo wangu anautesa usiku kucha ni presha
Hivi kwanini nimempenda
Laiti ningejua mbali nae ningeenda
Sina la kufanya nimekua wake mateka



No comments:

Post a Comment