Shughuli
ya kutekeleza hukumu kwa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa nchini
Zimbabwe imelazimika kusitishwa kwa sababu nchi hiyo haina mnyongaji.
Suala hilo limeibuka wakati wa kusikilizwa kwa shauri kwenye mahakama ya
kikatiba. Wafungwa waliohukumiwa kunyongwa wamehoji kuwa, kuwekwa
gerezani kwa muda mrefu bila adhabu waliopewa kutekelezwa ni kinyume cha
haki za binaadam. Wamesema, hukumu zao za kifo hazina budi sasa
kubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha. Wakati wa kusikiliza shauri
hilo, mwendesha mashtaka wa serikali amekiri kuwa hakuna mtu
aliyejitokeza kuomba nafasi ya kazi ya kuwa mnyongaji. Hukumu ya shauri
hilo kwenye mahakama ya kikatiba bado haijatolewa.
No comments:
Post a Comment