Saturday, January 30, 2016

SAED KUBENEA ADAI WABUNGE WANAWAKE WAVULIWA SHANGA ZAO NA POLISI



Image result for SAED KUBENEA 
SAED KUBENEA ADAI WABUNGE WANAWAKE WAVULIWA SHANGA ZAO NA POLISI

Mbunge wa jimbo la ubungo ameibua mpya tena bungeni baada ya wabunge wa chama pinzani kuondolewa na polisi nje ya ukumbi wa bunge.
Wabunge wa chama pinzani maarufu kama ukawa waliondolewa ndani ya ukumbi baada ya kugomea pendekezo la serikali lililoletwa na waziri mwenye dhamana  Nape Nauye kua mikutano ya bunge isionyeshwe live na TBC na badala yake irekodiwe na ionyeshwe usiku.
Baada ya kutoafikiana na wabunge wa upinzani kuchachamaa mwenyekiti wa bunge  Andrew Chenge aliamuru polisi kuwatoa nje wabunge hao. Kwa mujibu wa  saed kubenea akitoa malalamiko yake bungeni alidai kua wabunge wanawake walivuliwa nguo zao za ndani na kuvuliwa shanga zao na polisi.

Rais Magufuli Awaapisha Balozi Na Makatibu Tawala Wawili.....

Rais Magufuli Awaapisha Balozi Na Makatibu Tawala Wawili.....Amtuea Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mnadhimu Mkuu JWTZ


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Januari, 2016 amewaapisha Balozi, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania na Makatibu Tawala wawili, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Walioapishwa ni:
Balozi Mahadhi Juma Maalim, ambaye anakuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Kuwait.

Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, ambaye anakuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba, ambaye amestaafu. Kabla ya Uteuzi huu Luteni Jenerali Mabeyo alikuwa Mkuu wa Usalama na Utambuzi wa Jeshi la wananchi Tanzania.
Kamishna Paul Moses Chagonja, ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, akijaza nafasi iliyoachwa wazi Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Kamishna Clodwig Mathew Mtweve, ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, akijaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Balozi Mpya wa Tanzania nchini Kuwait Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim, ameahidi kuiwakilisha vyema Tanzania nchini Kuwait hususani katika uchumi ili Tanzania iweze kunufaika na ushirikiano uliopo baina ya mataifa haya mawili.

Nae Mnadhimu Mkuu wa Jeshi wa wananchi Tanzania Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, ameahidi kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na Mtangulizi wake Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Albert Ndomba ya kuhakikisha anamshauri vizuri Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na hivyo kuliwezesha Jeshi hilo kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Kwa upande wao, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Kamishna Clodwig Mathew Mtweve na Katibu wa Mkoa wa Katavi Kamishna Paul Moses Chagonja, wameahidi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwenye mikoa waliyopangiwa, ikiwemo kusimamia nidhamu kwa watumishi wa umma.

Gerson Msigwa,
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
30 Januari, 2016 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016

Nchi 12 Za Ulaya na Marekani Zalaani Tume Ya Uchaguzi Zanzibar

Nchi 12 Za Ulaya na Marekani Zalaani Tume Ya Uchaguzi Zanzibar Kutangaza Tarehe Ya Marudio Ya Uchaguzi Wakati Mazungumzo Yakiendelea


Mabalozi wa nchi zinazounda Umoja wa Ulaya (EU) wameeleza kusikitishwa na kitendo cha Tume ya Uchaguzi (ZEC) kutangaza tarehe ya marudui ya Uchaguzi wakati mazungumzo ya kutatua mgogoro yakiendelea na kumtaka Rais John Magufuli kutumia nafasi yake ya uongozi kutatua mtanziko wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Taarifa ya pamoja iliyotumwa kwa vyombo vya habari na mabalozi hao jana, pia inamtaka Rais Magufuli kuendeleza wito wake wa kuzitaka pande zote zitafute suluhu kwa amani.

Tamko hilo limetolewa siku saba baada ya mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha kutangaza kuwa uchaguzi wa rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani utarudiwa Jumapili ya Machi 20, lakini siku tano baadaye CUF ilitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio.

Kutokana na sakata hilo, mabalozi hao wamelaani kitendo hicho wakisema kurudia uchaguzi kwa kigezo kuwa utaratibu ulikiuka, kinawatia wasiwasi kwa kuwa tume hiyo haikutoa ushahidi wa ukiukwaji huo.

Mabalozi hao wamesema katika tamko lao kuwa ZEC imerudia kauli yake ya kuwa uchaguzi ulikiuka taratibu licha ya waangalizi kutoka EU, Jumuiya za Afrika Mashariki, Sadc Marekani na Jumuiya ya Madola kufanya tathmini na kujiridhisha kuwa ulikuwa huru na haki.

“Tunasikitika kuwa ZEC imetangaza tena kuwa uchaguzi utarudiwa Zanzibar, wakati mazungumzo baina ya pande mbili yanaendelea. Kwa manufaa ya Watanzania wote, tunasisitiza kuwa hali ya kisiasa ya visiwani humo ni bora ikatatuliwa kwa pande mbili kukubaliana,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyotumwa kwa ushirikiano wa mabalozi wa Uholanzi, Norway, Hispania, Italia, Ujerumani, Finland, Ufaransa, Sweden, Uswisi, Uingereza, Ireland na Marekani inasisitiza kuwa kitendo cha upande mmoja kuamua kurudia uchaguzi, kinaweza kuzidisha hofu na taharuki miongoni mwa Wazanzibari.

“Tunawaomba Wazanzibari kuwa watulivu na wavumilivu nyakati hizi na tunazitaka pande zote mbili na washirika wao kuendelea kufanya kazi pamoja ili wapate suluhisho la amani,” ilisema taarifa hiyo.

Pia inasema ili uchaguzi uwe wa kuaminika, mchakato wake hauna budi kuziwakilisha pande zote na kuwa huru na wa haki.

Hata hivyo, mabalozi hao wamesema kulingana na mazingira ya Zanzibar kwa sasa, itakuwa vigumu kwa waangalizi wa kimataifa kutegemewa kushiriki kwa namna yoyote katika uchaguzi huo.    

CCM Yaipongeza ZEC Kutangaza Tarehe Ya Marudio Ya Uchaguzi Zanzibar .....

CCM Yaipongeza ZEC Kutangaza Tarehe Ya Marudio Ya Uchaguzi Zanzibar .....Yawataka Wananchi Kujitokeza Kwa Wingi Kupiga Kura



CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar  kimeelezea kuridhishwa kwake na maamamuzi ya Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kutangaza siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani.

Kimesema  maamuzi  ya kufanyika uchaguzi huo Machi 20 mwaka huu, yanaenda sambamba na matakwa ya wananchi waliokuwa wengi katika kutekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa mujibu wa miongozo ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu alisema kwamba CCM inaungana na vyama vingine vya kisiasa nchini vilivyobaini kasoro za uchaguzi mkuu uliopita kuwa na kasoro na kuunga mkono maamuzi ya ZEC kuwa ni sahihi kwani yamefuata hatua muhimu za Kikatiba.

Waride alisema msimamo wa CCM katika Mkwamo wa kisiasa uliopo Zanzibar ni kurudi katika uchaguzi wa marudio ili kila chama cha kisiasa kinachoshiriki katika uchaguzi uliopita kipate haki ya kungia madarakani kwa njia halali na zinazokubalika kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo  Waride alieleza kwamba maamuzi hayo ndiyo kipimo sahihi cha kuweka uzani wa ukomavu wa kisiasa na demokrasia katika mfumo wa vyama vingi kwani lazima kila chama chenye haki ya kushiriki katika uchaguzi kiridhike na hatua zote zinazofanywa mpaka kupatikana kwa mshindi anayeongoza  kwa wingi wa kura halali.

“ Tunachukua fursa hii kuwaomba wananchi wote wenye haki ya kupiga kura hasa wafuasi wa CCM pamoja na wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura  Machi 20 mwaka huu.

"Tukumbuke kwamba maamuzi hayo yamefanywa na Chombo chenye Mamlaka ya kusimamia masuala yote ya Uchaguzi nchini baada ya kujiridhisha kuwa kuna kasoro zilizotokea katika uchaguzi uliofutwa na kuona kuna haja ya kila mwananchi kupata haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa njia huru, wazi na zinazokubalika kisheria”. Alifafanua Waride na kuongeza kuwa uchaguzi huo ndiyo njia mwafaka ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar.

Katibu huyo aliongeza kwamba pia wanaunga mkono msimamo wa vyama vya vyote vya kisiasa vilivyokubali kushiriki uchaguzi wa marudio pamoja ushauri wa Msajili wa Vyama vya Sisasa nchini, Francis Mtungi kwa kuvitaka vyama vyenye usajili kushiriki katika mchakato huo ili kudumisha Demokrasia na malengo na malengo ya vyama kutumia uchaguzi kushika Dola.

Akizungumzia suala la CUF kususia Uchaguzi wa marudio alisema kwamba walichofanya ni mwendelezo wa migomo na kususa kwa mipango  ya maendeleo inayofanywa na mamlaka za serikali katika kufanya mipango mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wananchi, hivyo hakuna jipya wala athari inayoweza kuathi hali ya kisiasa Zanzibar.

Alisema kwamba upinzani wa aina hiyo hauna nia njema ya kujenga maendeleo ya nchi bali una nia malengo ya kukwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoweka mbele tamaa ya madaraka kuliko maisha ya wananchi.

“ Kila chama kina sera zake na misimamo yake sasa wao kama wameona kususia uchaguzi wa marudio ndiyo njia ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar hiyo ni juu yao,  lakini sisi tutashiriki kikamilifu ili chama chetu kipate ridhaa ya wananchi kurudi madarakani ya kidemokrasia."

Aidha alisema  chama hicho kinaamini kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 mwaka 2015 ulikuwa na kasoro nyingi zilizosababisha uchaguzi huo kukosa sifa ya kuwa uchaguzi huru na wa haki na hatimaye kufutwa.

Kupitia taarifa hiyo Waride wamewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara wa mikoa minne kichama ya Unguja katika uzinduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM itakayofanyika katika  Afisi kuu ya CCM Kisiwandui, January 31 mwaka huu.

Alisema Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.
Mpekuzi blog

LHRC Yaitaka Serikali Kuheshimu Haki ya Watanzania Kupata Taarifa, Yalaani Wabunge Kudhalilishwa na Mbwa wa Polisi

Serikali imetakiwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kuwapa wananchi habari na taarifa muhimu zinazowahusu bila ya kujali gharama za taarifa hizo kwa kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na kituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake Bi. Imelda Urio na kuongeza kuwa kusitishwa baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kwa kisingizio cha gharama ni kitendo cha makusudi kwa kuwanyima wananchi taarifa muhimu toka kwa wawakilishi wao ambao ni wabunge.

Bi Imelda Urio ameongeza kuwa muhimili wa bunge na viongozi wake lazima wafanye kazi kiueledi na kuzuia mianya ya kuingiliwa na mihimili mingine hususani serikali.

Aidha LHRC imelaani vikali kitengo cha kuzalilishwa kwa wabunge kwa kutolewa bungeni na mbwa wa jeshi la polisi,

Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa utetezi na maboresho Bi. Anna Henga yeye amesema kuwa haki yoyote haina gharama na ni jukumu la serikali kulipia gharama hizo za matangazo ya bunge.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 30




Friday, January 29, 2016

Serikali Yakubaliana na Hoja ya Zitto Kabwe......Yauondoa Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano Bungeni

Serikali Yakubaliana na Hoja ya Zitto Kabwe......Yauondoa Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano Bungeni


Serikali imeamua kuondoa hoja yake ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano iliyokuwa imeuawasilisha mapema leo bungeni baada ya kudaiwa kuwa kilichowasilishwa hakikuwa mpango wa miaka mitano bali mwelekeo wa mpango wa mwaka mmoja.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wabunge Tundu Lissu na Zitto Kabwe kupinga mjadala wa hoja hiyo katika kikao cha leo mchana kuwa hakuna haja ya kuendelea na mjadala hadi serikali ipeleke mpango wa miaka mitano ukiambatana na muswada wa sheria husika.

Katika kikao hicho, ilipelekea mwenyekiti wa bunge Andrew Chenge kuahirisha kikao baada ya kambi ya upinzani kugoma kutoa maoni yake kupitia kwa mbunge David Silinde, na kupangwa kikao hicho kingeendelea jioni.

Katika kikao cha jioni, Mwenyekiti wa bunge alilazimika kuahirisha bunge hadi Jumatatu ijayo baada serikali kukubali kuondoa hoja yake kwa ajili ya kujipanga upya.


Umoja wa Vijana Chadema Wampa siku Tatu Rais Magufuli



BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kwa kushirikiana na Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu Chadema (Chaso) wametoa siku tatu kwa Rais John Magufuli kufuta agizo la Shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja mikutano ya Bunge inayoendelea Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi Taifa Bavicha Edward Simbeyi amesema, kitendo kilichofanywa na Serikali ni udikteta na kwamba, inawanyima wananchi kupata haki yao ya msingi.

“Tunajiuliza maswali mengi, ni vitu gani wanataka kuficha? Hadi wananchi wasivijue? Wakati Bunge linatakiwa kuwa masaa matano na dakika 45 sasa kwanini wanataka kurusha ndani ya saa moja? Haya masaa manne yanaenda wapi? Amehoji Simbeyi."

Amesema hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara yake ya 18 inatoa uhuru wa kila raia kupata au kupewa habari bila ya mashariti kama haya tunayoletewa leo.

“Wanaiogopa mijala inayoendelea Bungeni, Serikali yoyote inayoogopa kukosolewa lazima itakuwa na mapungufu yake, tunachohitaji ni mikutano uoneshwe live kila mtu ajue kinachoendelea” amesema Simbeyi.

Mbali na hilo, wameitaka serikali kutotumia ubabe ndani ya Bunge kwa lengo la kutaka kuwadhalilisha wabunge wa upinzani, pia Jeshi la polisi lizingatie maadili katika utendaji wao wa kazi na wasikubaliane na kila wanalotumwa na CCM hata kama linavunja sheria.

Amesema kitendo cha Jeshi la polisi kujiingiza katika masuala ya kisiasa ni kujidhalilisha wao wenyewe na ni hali inayoendelea kuwafanya kupoteza uaminifu wao ndani ya jamii

MAGAZETINI LEO

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Januari 29