Saturday, February 27, 2016
TANESCO Yapeleka Maombi ya Kupandisha Bei Ya Umem
TANESCO Yapeleka Maombi ya Kupandisha Bei Ya Umeme
SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limepeleka maombi kwa Mamlaka ya Udhibiti
wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kuomba kupandisha bei ya nishati
hiyo, kinyume na matakwa ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo ya kushusha bei hiyo.
Taarifa ya Ewura kwa umma iliyotolewa kwenye vyombo vya habari jana,
imeeleza kuwa maombi hayo yamepokewa Jumatano ya wiki hii na kutaka
wadau kujitokeza kujadili uhalali wa nyongeza hiyo siku mkutano huo
utakapoitishwa.
“Mamlaka inaanzisha mchakato wa kupata maoni ya wadau, ili kujua
uhalali wa maombi ya nyongeza ya bei za huduma iliyoyapokea kutoka
Tanesco,” imeeleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Tanesco iliwasilisha ombi husika
kulingana na Sheria ya Umeme namba 131, inayoitaka Ewura kufanya
mabadiliko ya bei zinazotozwa na mtoa huduma mara moja kila baada ya
miaka mitatu.
“Pendekezo la wastani wa badiliko la bei za umeme ni asilimia 1.1
kuanzia Aprili mosi 2016 na asilimia 7.9 kuanzia Januari mosi 2017,”
limeeleza tangazo hilo.
Mapendekezo hayo japo ya kisheria, lakini yanapingana na msimamo wa
Waziri Muhongo, ambaye tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo, alielezea
kusudio lake la kutaka bei ya nishati hiyo ishushwe.
Profesa Muhongo alikwenda mbali na kuagiza Tanesco, Ewura na Shirika
la Maendeleo ya Petroli (TPDC), kumpelekea mapendekezo ya kushuka kwa
bei ya umeme kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.
Katika maagizo hayo, Profesa Muhongo alihoji kwa nini bei ya umeme
isishuke, wakati gharama za uzalishaji wa umeme wa kutumia mafuta
zimeshuka kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.
Kutokana na maombi hayo ya Tanesco, Ewura imewataka wadau wa nishati
wanaopenda kutoa maoni yao kwa maandishi, kufanya hivyo kwa kutuma maoni
yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, ghorofa ya saba jengo la LAPF
Pensions Fund Tower, mkabala na Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama Dar
es Salaam.
Kwa watakaotuma kwa njia ya posta, wameombwa kufanya hivyo kwa
kutumia Sanduku la Posta 72175, Dar es Salaam, Tanzania, simu namba
(+255-22) 2123853-4; Fax namba (+255-22) 2123180; Barua pepe info@energyregulators.org au tovuti http://www. energyregulators. org.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mamlaka hiyo pia, itaitisha mikutano ya
wazi ili kukusanya maoni kuhusu mapendekezo hayo kutoka kwa wadau
mbalimbali, wakiwamo Baraza la Wawakilishi wa Watumiaji wa Huduma (CCC);
Baraza la Ushauri la Serikali (GCC) pamoja na wananchi kwa ujumla.
Majambazi Dar es Salaam Yavamia Benki Ya Access
Majambazi Dar es Salaam Yavamia Benki Ya Access....Yaua Mlinzi na Kupora Pesa, Polisi Wapambana Nayo na Kuyaua
Majambazi
ambao idadi yao haikufahamika wakiwa na mabomu na bunduki za
kisasa jana walivamia Benki ya Access tawi la Mbagala ambako
walipora viroba vya fedha, kuua mlinzi na baadae wanne kati yao
waliuawa na jeshi la polisi.
Watu
walioshuhudia tukio hilo walisema baada ya majambazi hao
kufika katika benki hiyo kwa bodaboda nne majira ya saa nane
mchana,yalimuua mlinzi wa benki hiyo, kusha kubomoa kwa risasi
mlango wa vioo na kuingia ndani na kuzua taharuki kubwa
Mashuhuda
hao walisema, katika tukio hilo lililodumu kwa karibu saa
moja,mmoja wa majambazi hao aliyekuwa amevaa kininja,alikuwa
barabarani akiamuru magari kupita haraka huku akifyatua risasi
hovyo.
Ilielezwa
kuwa, jambazi huyo aliyeonekana kuwa na uzoefu wa matumizi ya
bunduki alikuwa akifyatua risasi kwa kutumia mkono mmoja na
ndiye aliyewajeruhi baadhi ya wapita njia.
Hivyo,wakati
uporaji ukiendelea na jambazi huyo akiimarisha ulinzi
barabarani baadae hakukuwa na magari wala pikipiki zilizokuwa
zikipita.
Mfanyabiashara
wa duka la vifaa vya ujenzi jirani na benki hiyo,Ramadhani
Tairo alisema baada ya jambazi huyo kuliona gari la polisi
likielekea eneo la tukio,alifyatua risasi na kulipiga kabla
halijafika.Gari hilo lilipoteza mwelekeo na kutumbukia mtaroni.
Tairo
alisema mbali na jambazi huyo kulipiga risasi gari la polisi
pia alilirushia bomu la mkono,lakini liliangukia barabarani bila
kuripuka.Polisi walifanikiwa kulilipua bomu hilo baadae likiwa
halijasababisha madhara kwa wananchi waliofika kushuhudia tukio
hilo.
Mkazi
mwingine wa eneo hilo,Rebecca Maliva alisema majambazi
walioingia ndani ya benki hiyo walioneka wakitoka na viroba
vitatu vya fedha ambavyo walivipakata kwenye pikipiki na kuondoka
kwa kasi kuelekea Mkuranga kupitia barabara ya Kilwa.
Rebecca
alisema polisi zaidi walifika kwenye eneo hilo wengine wakiwa
kwenye pikipiki na kuanza kuwafukuza majambazi hao ambapo
walipofika eneo la shule ya St. Marry's,walitupa kiroba kimoja
cha fedha ambacho wananchi waliokuwa jirani waligombania na
kuchukua fedha zilizokuwemo na kisha kila mmoja kukimbia na
burungutu la noti.
Baada
ya nusu saa wakati umati ukiwa bado upo kwenye benki
hiyo,magari ya polisi yalipita katika eneo hilo yakitokea eneo
la Mkuranga yakiwa yamebeba miili ya majambazi yaliyouawa.
Magari hayo yalikuwa yakisindikizwa na vijana wa bodaboda waliokuwa wakishangilia kazi iliyofanywa na polisi.
Kamanda
wa p[olisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro
alizungumzia kwa ufupi tukio hilo n kwamba majambazi manne
yaliuawa na kukamata silaha tatu,lakini hakutaka kuingia kwa
ndani akisema atatoa taarifa zaidi leo
Friday, February 26, 2016
KUFUTWA KWA KIBALI KILICHOANZISHA CHUO KIKUU CHA MT. YOSEFU TANZANIA ( SJUIT) KAMPASI YA ARUSHA
Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania
TAARIFA KWA UMMA
1.
Tunapenda kuuarifu umma kwamba, Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania
(SJUIT)
Kampasi ya Arusha
ni mojawapo y
a vyuo vikuu vilivyosajiliwa na Tume ya
Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
ambacho kilianza kudahili wanafunzi kwa mara ya
kwanza mwaka wa masomo 2013/2014.
2.
Kwa mujibu wa kifungu cha
5(1)
cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya 346 ya Sheria
za Tanzania, Tume ina mamlaka
ya kusimamia na kudhibiti ubora na usimamizi
wa uendeshaji wa Vyuo Vikuu hapa nchini.
3.
Kwa muda mrefu na k
wa
w
akati tofauti
kumekuwapo na matukio ya migogoro
baina ya uongozi wa Chuo
Kikuu cha Mt. Yosefu Kampasi ya
Arusha
na
wan
afunzi.
Kwa kipindi hiki ch
ote
Tume imekuwa ikifuatili
a kwa karibu chimbuko
la migogoro hiyo na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutoa
maelekezo kwa uongozi wa chuo kurekebisha kasoro zinazosababisha
migogoro
chuoni hapo.
Kwa sehemu kubwa migogoro hiyo imekuwa ikitokana
na
matatizo ya ubora, uongozi, ukiukwaji wa sheria na taratibu za uendeshaji
wa chuo kikuu kama zilivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu. Hata hivyo
jitihada za Tume ya Vyuo Vikuu kukitaka Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania
(SJUIT) Kampasi ya Arusha kuhakikis
ha k
uwa elimu inayotolewa katika Ka
m
p
asi
hii inakidhi viwango vya ubora vilivyowekwa na Tume hazikupewa uzito stahiki
na uongozi wa chuo.
4.
Hivi sasa Kampasi ya Arusha ina jumla ya wanafunzi
1557
wanaosoma programu
za
masomo ya ualimu wa sayansi
zifuatazo:
2
Jina la Programu ya Masomo
Muda
wa
Masomo
Idadi ya
Wanafunzi
Bachelor of Science in Education with
Mathematics
& Chemistry
5
96
Bachelor of Science in Education with
Mathematics
& C
omputer
S
cience
5
36
Bachelor of Science in Education with Physic
s
&
Mathematics
5
40
Bachelor of Scie
nce in Education w
ith
Physics & Chemistry
5
74
Bachelor of Science in Education
with
Physics &
C
omputer
S
cience
5
4
Bachelor of Science in Education with
Biology & Chemistry
5
237
Bachelor of Science in Education with Mathematics
& Chemistry
3
103
Bachelor of Science in Education with
Mathematics
& C
omputer
S
cience
3
119
Bachelo
r of Science in Education with
Physics &
Mathematics
3
69
Bachelor of Science in Education with
Physics & Chemistry
3
254
Bachelor of Science in Education with
Physics &
C
omputer
S
cience
3
28
Bachelor of Science in Education with
Biology & Che
mistry
3
497
Jumla
1557
5.
Kutokana na yaliyobainishwa hapo awali, tunapenda kuuarifu umma kwamba,
Tume imejiridhisha kuw
a
Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu
Tanzania imepoteza sifa na vigezo vya kuen
delea kutoa elimu ya chuo kikuu.
K
wa kuzingatia ukweli kwamba wanafunzi ndio waathirika wakuu wa matatizo
yaliyopo kwenye
Kampasi hii
,
Tume
imeamua kama ifuatavyo:
a)
I
me
futa kibali kilichoanzisha
Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt.
Yosefu Tanzania (SJUIT)
na kuidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote
waliokuwa wanasoma katika
K
a
mpasi hiyo
ya Arusha
kwa gharama za Chuo
Kikuu cha SJUIT.
Orodha ya majina yao na vyuo wataka
vyopangiwa
itatangazwa na kuwekwa katika tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu hivi punde.
b)
Imefuta udahili wa wanafunzi wapya katika programu ya shahada ya miaka
mitano ya ualimu wa sayansi.
Na kwamba, wanafunzi wanaoendelea na
masomo katika programu hii watahamis
hiwa katika Kampasi ya
Luguruni,
Dar
es Salaam
, na watalazimika kwanza ku
hitimu katika ngazi ya Stashada
(Diploma)
kama ilivyokuwa imeidhin
i
shwa
na Tume
hapo awali.
Utaratibu wa
Thursday, February 25, 2016
Gesi Nyingine Yagundulika Bonde la Mto Ruvu....Ina Ukubwa wa Ujazo wa Futi Trilioni 2.17
Tanzania
imedhihirisha kuwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi asilia baada
ya kugundulika kwa gesi nyingine katika bonde la mto Ruvu yenye ukubwa
wa ujazo wa futi trilioni 2.17.
Ugunduzi
huo wa gesi asilia umefanywa na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons and
Power Tanzania Limited ambayo imekuwa inafanya shughuli za utafutaji wa
gesi na mafuta katika Mkoa wa Pwani.
Mtendaji
Mkuu wa kampuni hiyo, Pilavullathil Surendran alisema jana katika
mkutano wa wawekezaji wa gesi na mafuta ulioandaliwa na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwa, thamani ya gesi
iliyoko katika eneo hilo inafikia Dola za Marekani bilioni sita sawa na
Sh trilioni 12.
Ugunduzi huo mpya unafanya hadi sasa Tanzania kuwa na amana ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.
Kwa
upande wake, Profesa Muhongo alithibitisha kugundulika kwa gesi hiyo
tangu Julai mwaka jana, lakini akaeleza kuwa Serikali imechelewa
kutangaza ugunduzi huo kama inavyoagizwa na Sheria ya Mafuta ya Mwaka
2015 kutokana na shughuli za uchaguzi.
“Sheria
mpya inatutaka kabla ya waziri mwenye dhamana ya gesi kutangaza
ugunduzi mpya wa gesi na mafuta ni lazima athibitishiwe na mamlaka ya
udhibiti wa bidhaa za Petroli na Gesi (PURA).
“Wizara
yangu itawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kupata ushauri
wa kisheria kuhusu jambo hilo na bahati nzuri tayari PURA imeshaanza
kushughulikia jambo hilo na naamini kuwa nitatangaza ugunduzi huo mpya
hivi karibuni,” alifafanua Profesa Muhongo.
Licha
ya ugunduzi huo mpya tayari gesi imegundulika katika maeneo ya kisiwa
cha Songo Songo mkoani Lindi na eneo la Mnazi Bay huko Mtwara na katika
Wilaya ya Mkuranga, Pwani pia kumegundulika kiasi kikubwa cha gesi.
Subscribe to:
Posts (Atom)