RC Makonda Aitisha Kikao na Walimu ili Kujadili Matatizo Yanayowakabili
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paulo Makonda amemwagiza Ofisa
Elimu,Raymond Mapunda kuitisha mkutano wa walimu March 26 mwaka
huu ili kujadili matarizo yanayowakabili likiwemo la kutopanda
madaraja kwa wakati.
Makonda
aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akikabidhi madawati
500 katika shule ya msingi Kawawa yaliyotolewa na kampuni ya
simu za mkononi ya Tigo.
Mkuu
huyo alieleza kuwa yapo matatizo mengi yanayowakabili walimu
yanayotokana na watu wanaojinufaisha matumbo yao kwa kuwalipa walimu
hewa
Katika hatua nyingine,Makonda aliwataka walimu kutovunjwa moyo kutokana na matatizo yaliyopo katika sekta ya Elimu.
Naye
mkurugenzi wa kampuni ya Tigo,Diego Gutierrez alisema kuwa mchango huo
ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni ya Tigo kuunga mkono
jitihada za serikali katika kuleta maendeleo ya elimu nchini
No comments:
Post a Comment