Bomu Lalipuka Maskani ya CCM Zanzibar
Kitu
kinachosadikika kuwa bomu kimeripuka usiku wa kuamkia jana eneo la
Michenzani mjini Unguja, eneo linalojulikana kama maskani maarufu ya
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mlipuko
huo umezua taharuki na hofu kwa wananchi wa eneo hilo hususan wanachama
wa CCM ambao hukutana kwa wingi eneo hilo na kujadili masuala
mbalimbali ya chama chao kuelekea uchaguzi wa marudio uliopangwa
kufanyika Machi 20 mwaka huu.
Naibu
Katibu Mku wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alilaani tukio hilo na
kulielezea kuwa liliandaliwa makusudi kwa lengo la kuwavunja moyo
wanachama wa chama hicho.
“Hili
sio tukio la kwanza wala la pili katika eneo hili ambalo wanachama wetu
walio msitari wa mbele wako wengi sana kwa kushirikiana na wanachama
wengine.
"Hili
ni tukio ambalo unaweza kusema limeandaliwa kwa makusudi na watu wenye
dhamira ya kuwavunja moyo wanachama wetu na wapenzi wa CCM,” Vuai aliwaambia waandishi wa habari.
Naye
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibu, Mkadam Khamis Mkadam
alieleza kuwa Jeshi hilo liliwasili katika eneo hilo usiku huo na
kuimarisha ulinzi hadi asubuhi.
Kamanda
Mkadam alisema kuwa walichukua vipande vya mlipuko huo na kuvipeleka
sehemu husika kwa ajili ya kuchunguza kubaini aina ya mlipuko huo na
vifaa vilivyotumika
No comments:
Post a Comment