Sunday, March 6, 2016
Breaking News : Rais Magufuli Amteua Balozi John Wiliam Kijazi Kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.......Ombeni Sefue Atapangiwa Kazi Nyingine
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua
Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.
Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment