Sunday, March 13, 2016
Katibu Mtendaji NACTE Ajiuzulu....Ni Kutokana na Tuhuma za Kughushi Vyeti
==>Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa NACTE Dokta Primus D Nkwera (kulia) akifafanua jambo
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Vyuo vya Ufundi( NACTE),Dr. Primus Nkwera amejiuzulu nafasi yake.
Uamuzi
wa kujiuzulu kwa Dr. Nkwera ulitangazwa katika ofisi kuu za Baraza
hilo zilizopo Mikocheni Dar es Salaam juzi na Mwenyekiti wa
Bodi,Mhandisi Steven Mlote na kusababisha baadhi ya wafanyakazi
kuangua kilio.
Akizungumza
katika kikao cha dharura cha wafanyakazi wote wa baraza hilo,Mlote
alisema Dr. Nkwera amejiuzulu ili kulinda hadhi ya Nacte kutokana
na habari iliyoandikwa na Gazeti la Dira ikimtuhumu mambo mbalimbali.
Gazeti
hilo la Dira la Jumatatu tarehe 07/03/2016 toleo no.405 lilimtuhumu
Katibu Mtendaji wa NACTE, Dr.Primus Nkwera kughushi vyeti vya shahada
ya uzamivu baada ya kusomeshwa na serikali Afrika Kusini na kufeli.
Mlote
alisema kwa mujibu wa Dr. Nkwera, nafasi hiyo haipaswi kushikwa na mtu
mwenye tuhuma ya aina yoyote, na ametafakari na kuona ajiweke kando
na uongozi wa Nacte ili uchunguzi ufanyike akiwa pembeni.
"Tumetumia muda mwingi kutafakari hoja ya Dr. Nkwera na hatimaye tumekubali kujiuzulu kwake kwa shingo upande," alisema Mlote na kuongeza:
"Kazi
kubwa iliyofanywa na Dr. Nkwera akiwa kiongozi wa Nacte inafahamika na
kila mmoja, vilio na machozi ya wafanyakazi wenzake yanadhihirisha kuwa
kujiuzulu kwake kunaacha simanzi kubwa.
"Najua
mmepata mshtuko mkubwa, lakini Dr Nkwera hajafa, yuko hai na huyu bado
ni mtumishi wa serikali. Alichofanya ni kuamua kuachana na ukatibu
utendaji.
"Tutaendelea
kumtumia itakapobidi kwa ushauri.Wakati mwingine lazima mkubaliane na
hali hii, lakini pia endeleen kuchapakazi kwa ufanisi kama kawaida
kana kwamba bado mko na Dr. Nkwera."
Kutokana
na kujiuzulu kwake, Mlote alisema bodi imemteua Mkurugenzi wa Mitaala
wa Nacte, Dr Adolf Rutayunga kukaimu nafasi hiyo wakati taratibu
nyingine zikiendelea.
Akizungumza
na wafanyakazi hao, Dr. Rutayunga alisema viatu alivyoviacha Dr. Nkwera
ni vikubwa kwake, lakini akaahidi kuendeleza yote aliyoyaacha.
No comments:
Post a Comment