Mansoor Yussuf Himid Ambaye ni Mshauri wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Akamatwa Na Jeshi La Polisi
Jeshi la Polisi linamshikilia mwanasiasa Mansoor Yussuf Himid kwa mahojiano kuhusiana na kulipuliwa kwa maskani ya CCM, Kisonge Michenzani mjini Unguja.
Mansoor, ambaye ni mshauri wa Katibu Mkuu
wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad alipigiwa simu
jana jioni na polisi kwa ajili ya mahojiano katika kituo cha Madema.
Kukamatwa
kwa Mansoor kumekuja siku chache baada ya Jeshi hilo kuwakamata wafuasi
wengine 42 akiwamo Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya
Umma, Hamad Masoud akituhumiwa kutoa taarifa kwamba kuna watu
wamekimbilia porini na wengine wamekwenda Mombasa.
Wafuasi
hao 42 ambao bado wanashikiliwa ni kutokana na kuhusishwa na tukio la
kulipuliwa nyumba ya Kamishina wa Polisi, Hamdan Omar Makame.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam jana
alithibitisha kukamatwa kwa Mansoor na kwamba ni kutokana na hali ya
matukio ya milipuko na mambo mengine, hivyo wanahitaji kupata maelezo ya
kina kabla ya kumwachia.
Alisema
lengo la kumshikilia Mansoor si kumkomoa bali ni kupata ufafanuzi na
maelezo kwani hivi sasa kutokana na hali na matamshi ambayo huwa
yanatolewa katika mitandao ya kijamii, Jeshi la Polisi linayafuatilia
kwa kina kuyachunguza.
“Kwa
hivyo tunataka maelezo na tukishapata maelezo yake tutaamua kama ni
kumwachia au la, lakini kwa sasa tunamhitaji kwa kuisaidia polisi kwenye
upelelezi,” alisema Mkadam.
Tukio
hilo limekuja saa chache baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara,
Magdalena Sakaya kulalamikia dalili za wazi za uvunjifu wa haki za
binadamu Zanzibar zinazofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wafuasi wao
kwa kivuli cha utunzaji wa amani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Sakaya aliisihi
Serikali ya Rais John Magufuli kuingilia kati kwani wananchi wanaweza
kuchoshwa na vitendo hivyo na kuleta uvunjifu zaidi wa amani.
Sakaya alisema kuwa wanaamini mambo yote hayo yanatokea kutokana na msimamo wao wa kutokubali kushiriki uchaguzi wa marudio unaofanyika Jumapili hii.
Sakaya alisema kuwa wanaamini mambo yote hayo yanatokea kutokana na msimamo wao wa kutokubali kushiriki uchaguzi wa marudio unaofanyika Jumapili hii.
Uchaguzi
huo wa marudio unafanyika baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka
jana kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha
Salim Jecha kutokana na kile alichodai kukithiri kwa ukiukwaji wa
taratibu na sheria za uchaguzi.
Sakaya
alisema kuwa kuna vitendo vingi wanafanyiwa wafuasi wa CUF visiwani
humo vikiwamo vya kupigwa na vikundi vya uhalifu vinavyoitwa ‘mazombi’,
kuchomewa nyumba na kutiwa ndani kwa viongozi wa chama hicho kwa
visingizio vya kushiriki uhalifu.
No comments:
Post a Comment