Dr Slaa Afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni
Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.
Wawili
hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa moja, lakini
habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri
kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Ndoa
hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu za Dr Slaa ambaye mwaka 2010
aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani akidai bado
anamtambua Josephine kuwa ni mke wake wake halali.
Mume
huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama impatie
haki yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.
Misukosuko
ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa mke wake, Rose
Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.
Dr
Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi
kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa
kutokana na mapingamizi hayo.
No comments:
Post a Comment