Maandalizi ya Uchaguzi Visiwani Pemba Yakamilika....Wananchi Watakiwa Kujitokeza Kwa Wingi Kesho Kupiga Kura
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imesema maandalizi ya uchaguzi visiwani
Pemba yamekamilika na kuwataka wananchi kujitokeza kesho kupiga kura na
kuachana na dhana kuwa kutakuwa na vurugu.
Mwandishi wetu
alishuhudia malori saba ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) yakipakia
vifaa vya uchaguzi katika ofisi ya ZEC Pemba katika tukio lililowafanya
baadhi ya wananchi kuacha shughuli zao wakishangaa na wengine wakisema;
“sasa shughuli imeanza”.
Ofisa Mdhamini wa ZEC Pemba, Ali
Mohammed Dadi alisema wameshapokea karatasi na masanduku ya kupigia kura
na fomu mbalimbali.
Alisema karatasi za uchaguzi wa wawakilishi na
madiwani zilianza kusambazwa jana na walitarajia kupokea za urais jana
jioni na kuzisambaza leo.
Jana, magari 15 ya polisi aina ya Land
Rover yakiwa na askari 10 wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kila
moja, zilionekana zikirandaranda katika mitaa ya Pemba.
“Sisi
tunachotaka ni amani tu hao askari waje tu watulinde hakuna mfanya
vurugu hapa. Hata wakizagaa mtaani kwetu heri tu ili mradi wasituzuie
kufanya shughuli zetu, “alisema Ramadhani Hamisi Omar, mkazi wa
Chakechake.
No comments:
Post a Comment