Sunday, March 13, 2016

Katibu Mtendaji NACTE Ajiuzulu....Ni Kutokana na Tuhuma za Kughushi Vyeti

Sunday, March 13, 2016

Katibu Mtendaji NACTE Ajiuzulu....Ni Kutokana na Tuhuma za Kughushi Vyeti

==>Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa NACTE Dokta Primus D Nkwera (kulia) akifafanua jambo
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la  Elimu ya Vyuo vya Ufundi( NACTE),Dr. Primus Nkwera amejiuzulu nafasi yake.
Uamuzi wa kujiuzulu  kwa  Dr. Nkwera ulitangazwa katika ofisi  kuu  za Baraza  hilo  zilizopo  Mikocheni  Dar es Salaam juzi na Mwenyekiti  wa  Bodi,Mhandisi Steven Mlote na kusababisha  baadhi  ya  wafanyakazi  kuangua  kilio.
Akizungumza katika kikao cha dharura cha wafanyakazi wote wa baraza hilo,Mlote alisema Dr. Nkwera amejiuzulu  ili  kulinda  hadhi  ya Nacte kutokana  na  habari iliyoandikwa na Gazeti la Dira ikimtuhumu mambo mbalimbali.
Gazeti  hilo la Dira la Jumatatu tarehe 07/03/2016 toleo no.405 lilimtuhumu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dr.Primus Nkwera  kughushi vyeti vya shahada ya uzamivu  baada ya kusomeshwa na serikali Afrika Kusini na kufeli.

Mlote alisema kwa mujibu wa Dr. Nkwera, nafasi hiyo haipaswi kushikwa na mtu mwenye tuhuma  ya  aina  yoyote, na ametafakari na kuona ajiweke kando na uongozi wa Nacte ili uchunguzi ufanyike akiwa pembeni.

"Tumetumia muda mwingi kutafakari hoja  ya  Dr. Nkwera na hatimaye tumekubali kujiuzulu kwake kwa shingo upande," alisema Mlote na kuongeza:

"Kazi kubwa iliyofanywa na Dr. Nkwera akiwa kiongozi wa Nacte inafahamika na kila mmoja, vilio na machozi ya wafanyakazi wenzake yanadhihirisha kuwa kujiuzulu kwake kunaacha simanzi kubwa.

"Najua mmepata mshtuko mkubwa, lakini Dr Nkwera hajafa, yuko hai na huyu bado ni mtumishi wa serikali. Alichofanya ni kuamua kuachana na ukatibu utendaji.

"Tutaendelea kumtumia itakapobidi kwa ushauri.Wakati mwingine lazima mkubaliane  na  hali  hii, lakini pia  endeleen kuchapakazi kwa ufanisi kama  kawaida kana kwamba bado mko na Dr. Nkwera."

Kutokana  na  kujiuzulu  kwake, Mlote alisema bodi imemteua Mkurugenzi wa Mitaala wa Nacte, Dr Adolf Rutayunga kukaimu nafasi hiyo  wakati taratibu nyingine zikiendelea.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Dr. Rutayunga alisema viatu alivyoviacha Dr. Nkwera ni vikubwa kwake, lakini  akaahidi kuendeleza yote  aliyoyaacha.

Sunday, March 6, 2016

balozi ombeni sefue awekwa benchi

Sunday, March 6, 2016

Breaking News : Rais Magufuli Amteua Balozi John Wiliam Kijazi Kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.......Ombeni Sefue Atapangiwa Kazi Nyingine

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. 
Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi  wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam

Saturday, March 5, 2016

Waziri Mkuu Asema Mtu Akiharibu Kazi Asitarajie Uhamisho.

Waziri Mkuu Asema Mtu Akiharibu Kazi Asitarajie Uhamisho.



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa(Pichani) amesema watumishi wa umma wako huru kuhamia kokote wapendako lakini wahakikishe wanaenda huko wakiwa safi na kamwe mtu asiharibu kazi kazi akitarajia kuwa atahamishiwa sehemu nyingine.

"Serikali hii haina utumishi kwa mtu aliyeharibu kazi,usije ukaharibu hapa Itilima ukadhani utaenda Bunda kuendelea na kazi. Serikali ya awamu hii haina nafasi na  watumishi wa aina hiyo," amesema.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Ijumaa, Machi 4, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Itilima kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambao ameuzindua leo hii wilayani Itilima, mkoani Simiyu.

"Watumishi wenzangu huu ni wakati wa kubadilika na kuona mwelekeo wa Serikali hii ya awamu ya tano ukoje. Jukumu letu ni kuwatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi zao, rangi wala dini zao," alisisitiza.

Waziri Mkuu aliwahakikishia watumishi hao kwamba Serikali inatambua changamoto walizonazo kutokana na upya wa wilaya hiyo na mkoa huo na akawaahidi kuwa itaboresha mazingira yenu. 
"Msiwaadhibu wananchi kwa kisingizio cha mazingira magumu ya kazi zenu, tunajua mnayo madai ya nauli, posho za mafunzo, kupandishwa madaraja na malimbikizo ya likizo," alisema huku akishangiliwa.

Alisema Serikali itayalipa madeni hayo japo haitamaliza yote kwa wakati mmoja ila ana uhakika wa kukamilisha walau kwa asilimia 80.

Mapema, akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Bibi Georgina Bundala alisema wilaya hiyo iliyoanzishwa Machi 2012 na kupata Halmashauri Julai 2013 haina kituo cha polisi cha wilaya, haina gereza, Ofisi za TAKUKURU, mahakama ya wilaya wala benki.

Alisema wilaya hiyo haina hospitali ya wilaya ila akabainisha kuwa wamekwishatenga eneo la ekari 30 kwa ajili ya ujenzi huo.
 "Pia tumekwishapima viwanja 123 na eneo la kujenga  taasisi lenye ekari 143.8 limefanyiwa uthamini na fidia kukamilika," alisema.

magazetini leo

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 5


Bomu Lalipuka Maskani ya CCM Zanzibar

Bomu Lalipuka Maskani ya CCM Zanzibar

Kitu kinachosadikika kuwa bomu kimeripuka usiku wa kuamkia jana eneo la Michenzani mjini Unguja, eneo linalojulikana kama maskani maarufu ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mlipuko huo umezua taharuki na hofu kwa wananchi wa eneo hilo hususan wanachama wa CCM ambao hukutana kwa wingi eneo hilo na kujadili masuala mbalimbali ya chama chao kuelekea uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.

Naibu Katibu Mku wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alilaani tukio hilo na kulielezea kuwa  liliandaliwa makusudi kwa lengo la kuwavunja moyo wanachama wa chama hicho.

“Hili sio tukio la kwanza wala la pili katika eneo hili ambalo wanachama wetu walio msitari wa mbele wako wengi sana kwa kushirikiana na wanachama wengine. 
"Hili ni tukio ambalo unaweza kusema limeandaliwa kwa makusudi na watu wenye dhamira ya kuwavunja moyo wanachama wetu na wapenzi wa CCM,” Vuai aliwaambia waandishi wa habari.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibu, Mkadam Khamis Mkadam alieleza kuwa Jeshi hilo liliwasili katika eneo hilo usiku huo na kuimarisha ulinzi hadi asubuhi.
Kamanda Mkadam alisema kuwa walichukua vipande vya mlipuko huo na kuvipeleka sehemu husika kwa ajili ya kuchunguza kubaini aina ya mlipuko huo na vifaa vilivyotumika
==

Mkuu wa mkoa mwanza awapasua jipu walimu 8 kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Aamuru Kukamatwa Papo hapo Walimu 8 Kwa Kujihusisha na Mapenzi na Wanafunzi


Walimu wanane wa Shule ya Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi.

Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24, 2013.

Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel.

Walimu watatu waliokuwa wakifundisha shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga.

Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajili ya picha za kuweka kwenye vitambulisho (passport size).

Akitangaza uamuzi huo, Mulongo alisema tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa Januari 27, kuchunguza tuhuma dhidi ya walimu hao kujihusisha na mapenzi na wanafunzi imebaini ukweli baada ya kuwahoji wanafunzi kadhaa.

“Ni fedheha na haivumiliki kuona walimu wakifanya mapenzi na wanafunzi wao. OCD wakamate walimu wote na uanze uchunguzi mara moja na kukusanya ushahidi utakaowezesha wahusika kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,” aliagiza Mulongo.

Amri hiyo ilitekelezwa mara moja kwa walimu hao kuwekwa chini ya ulinzi.

Mulongo pia alimwagiza Katibu wa Idara ya Utumishi wa Walimu Mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani kuwaandikia barua za onyo walimu wa kike shuleni hapo kwa kushindwa kulinda na kutetea masilahi ya wanafunzi wa kike waliokuwa wakidhulumiwa kingono na walimu wenzao kiasi cha baadhi yao kuathirika kisaikolojia.

Pia, alimwagiza Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Khamisi Maulid kuangalia uwezekano wa kuwahamishia shule nyingine wanafunzi waliodhulumiwa kingono na walimu wao ili kuwaepusha na matatizo ya kisaikolojia.

Maulidi alisema wanafunzi walioathirika zaidi ni wale wa kidato cha nne.

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mkoa wa Mwanza, Said Mselem alisema kitendo hicho kimeifedhehesha taaluma ya ualimu na kuahidi kuwa ofisi yake itatanua wigo wa uchunguzi hadi kwenye shule nyingine. 

Thursday, March 3, 2016

Dr Slaa Afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni

Dr Slaa Afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni

Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.
Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa  moja, lakini  habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita. 
Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu  za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani  akidai bado anamtambua Josephine  kuwa ni mke wake wake halali.
Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama  impatie haki  yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.

Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa  mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.
Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa kutokana na mapingamizi hayo.
==