Ndiyo maana siku chache zilizopita nilisema:
i) Ni muhimu kwa "Mshenga Gwajima" kutubu na kuwaomba Radhi Watanzania kuliko kuendelea kuwapotosha.
ii) Mungu hamilikiwi na binadamu awaye yote. Watanzania tunawajibu wa
kumshukuru sana Mungu kwa kutukomboa na kutuokoa na " Mabadiliko" ya "
Kuzungusha Mikono". Mshenga na UKAWA yake walitaka kutuaminisha sote
kuwa Mabadiliko ni kuzungusha mikono! Walitaka kutuaminisha kuwa
"Mabadiliko ni Lowassa na Lowassa ni Mabadiliko".
Lowassa aligeuzwa kuwa "Ajenda" badala ya ajenda za Msingi za Wananchi.
Mungu amesikiliza Sala za Wanyonge na Walalahoi. Namshukuru sana Mungu
aliyenionyesha kuwa kati ya wawili hao, japo wote kila mmoja ana uchafu,
Magufuli ni "Nafuu mara eflu" kuliko fisadi Lowassa. Asante sana Mungu
Mwema kwa kulinusuru Taifa lako lililotaka kuingizwa "mjini" na makuwadi
kwa ulaghai na upotoshwaji uliopitiliza.
iii) Nilimtaka Gwajima awaombe radhi Maaskofu aliosema "wamehongwa na
Lowassa na kuwa fedha hizo waligawiwa mbele ya Mavho yake. Alisema bila
kumumunya maneno, kuwa.... Maaskofu wa ki lutheri alikwisha malizana
nao" na kuwa kati ya "Maaskofu wa Kikatoliki 34 wamehongwa Maaskofu 30
na kumtaja kwa jina Askofu Mkuu mmoja, ambaye yeye kapewa fedha za
kununulia gari la kiaskofu." Fedha hizo alidai zimetolewa na Lowassa
kupitia Rostam Azizi. Gwajima, Tambua kuwa kama ni kweli toka tena
hadharani wakemee Maaskofu wanaopokea Rushwa, na kama si kweli Waombe
Radhi hadharani Maaskofu hao kwani kauli hiyo ilitaka kuwagawa Maakofu
na kuwachafua.
Lakini, alitamka hayo akiona ni sifa, ndiyo maana nilimshangaa kiongozi
wa dini ambaye badala ya kukemea anaona ni sifa. Kama wenzangu
waliokuwepo na wao wana Misingi ya kusimamia basi watatoa ukweli wao, na
kama wanachukia ufisadi basi watatoka hadharani kukemea tamko hilo
lililotolewa mbele yetu watu 4 akiwemo Mshenga.
Nilipotamka hivi wengi walidhani Dr. Slaa ndiye Katamka kuwa Maaskofu
"Wamehongwa". Kama Askofu anaweza kufika mahali akawasingizia wenzake ni
hatari sana na halihitsji kufungiwa Macho na masikio. Kama anavyosema
Gwajima ni " kweli". Basi wote tunaopenda kupiga vita Ufisadi ni lazima
tupaze sauti zetu, na kukemea kitendo hicho kama kweli kimefanywa na
wale tunaotegemea kusimamia maadili katika Jamii yetu. Wako walioniambia
Dr. Slaa unapata wapi ujasiri wa kuwasema viongozi wa dini. Sijawahi
kuyumba wala kuyumbishwa. Ukweli utatamkwa hata kama ni mchungu, na uovu
na uozo utasemwa tu hata kama umetendwa na nani. Ukitazama nyuso za
wazi " haki haitatendeka milele.
iv) Katika busara ya kawaida, hatukutegemea Gwajima kujitokeza "Kumkana
Lowassa" hasa kabla ya kuomba radhi. Aidha Kauli " Live" kwenye YouTube
na mitandao mbalimbali ziko bado kibao. Ama kweli Gwajima ni kiongozi
asiye na dhamira kukanusha kauli zake hizo kabla ya kuomba radhi.
v) Wako watakaodhani kuwa Dr Slaa ana "bifu" binafsi na Gwajima. Ni
kweli kibinadamu nimeumia sana kwa kuwa kuumizwa na rafiki kunaumiza
sana, lakini nawaonea huruma zaidi Watanzania Waliobebwa kwa ushabiki
mkubwa na kupoteza nguvu zao nyingi na labda "kupoteza fursa ya kuiondoa
CCM kwa muda mrefu ujao" kwa kuwaamini watu kama kina Gwajima. Hiki
ndicho kinachonisukuma zaidi kuendelea kumkaba Gwajima hadi atakapoomba
radhi kwa watanzania wanyofu.
Nawaomba Watanzania tuwe na kumbukumbu. Tuzisikilize tena Kauli
mbalimbali alizozitoa Gwajima, tena wakati mwingine kwa njia ya Maombi
kwa jina la Mungu. Hali hii isipokemewa kwa ukali sana ni hatari sana.
Ndugu zangu wanaJF na Watanzania wote,
Pamoja na yote haya, ninawatakia Heri nyingi kwa sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2016 uwe wa Baraka na mafanikio.
By Dr .Slaa
No comments:
Post a Comment