Sunday, December 27, 2015

MCHUNGAJI WANGU GWAJIMA YULE MUNGU ALIYEMTAKA LOWASSA AMEBADILIKA??







Katika mambo tunayofundishwa katika makanisa yetu ni kuwa Mungu wetu habadiliki akisema ndiyo hakuna wa kusema hapana.
Katika kipindi cha kampeni kwa bahati mbaya viongozi wetu wa dini walijihusisha na siasa za moja kwa moja. Jambo lililotushangaza Wengi hasa sisi tusio na aibu ya kusema. Sisi tulisema wazi kuwa huko ni kupotoka tena kupotoka kiimani.
Sisi tuliamini kuwa kazi ya viongozi wetu wa dini katika kipindi cha uchaguzi ni kumwomba Mungu iliatupe kiongozi sahihi na atakayemtumikia Mungu kupitia utumishi wake kwa wananchi.
Kwa hali ya kushangaza baadhi ya viongozi wetu wa dini wao walipiga kampeni kwa baadhi ya wagombea wa urais.
Walituaminisha kuwa Mungu anamtaka lowassa na kusizitiza kuwa anayemkataa Edward anamkataa Mungu.
Na si viongozi wa dini tu mpaka vikundi vya kiroho viliingia katika mtego huu badala ya kumwomba Mungu atupe kiongozi wao walitaka lowassa.
Hivi karibuni Gwajima yaani mshenga wa lowassa kwa maneno ya dr. Slaa kamkana lowassa nakudai kuwa hakumpigia kampeni bali alikuwa katika mikutano ya ukawa kwa ajili ya kufanya sala. Swali ni kuwa je, aliyekuwa mgombea urais ni lowassa pekee??mbona hatukumuona akifanya sala katika mikutano ya akina Magufuli, Rungwe, Anna, Malik, chief yemba, au ya akina Lyimo??
Mchungaji wangu au huku kwa akina yemba hawakukutaka maombi??
Baba Mchungaji vipi leo yule uliyetuaminisha ni chaguo la Mungu umeamua kamkana....je, Mungu wetu ni kigeugeu???
MIMI NAAMINI MUNGU AKISEMA NDIYO HAKUNA WA KUZUIA,,,,,,MUNGU HAKUSEMA NDIYO KWA LOWASSA.....KAMA ANGESEMA ANGEMTETEA

DR. SLAA AMTAKA MSHENGA WA LOWASA AOMBE RADHI

 

Ndiyo maana siku chache zilizopita nilisema:

i) Ni muhimu kwa "Mshenga Gwajima" kutubu na kuwaomba Radhi Watanzania kuliko kuendelea kuwapotosha.
ii) Mungu hamilikiwi na binadamu awaye yote. Watanzania tunawajibu wa kumshukuru sana Mungu kwa kutukomboa na kutuokoa na " Mabadiliko" ya " Kuzungusha Mikono". Mshenga na UKAWA yake walitaka kutuaminisha sote kuwa Mabadiliko ni kuzungusha mikono! Walitaka kutuaminisha kuwa "Mabadiliko ni Lowassa na Lowassa ni Mabadiliko".

Lowassa aligeuzwa kuwa "Ajenda" badala ya ajenda za Msingi za Wananchi. Mungu amesikiliza Sala za Wanyonge na Walalahoi. Namshukuru sana Mungu aliyenionyesha kuwa kati ya wawili hao, japo wote kila mmoja ana uchafu, Magufuli ni "Nafuu mara eflu" kuliko fisadi Lowassa. Asante sana Mungu Mwema kwa kulinusuru Taifa lako lililotaka kuingizwa "mjini" na makuwadi kwa ulaghai na upotoshwaji uliopitiliza.

iii) Nilimtaka Gwajima awaombe radhi Maaskofu aliosema "wamehongwa na Lowassa na kuwa fedha hizo waligawiwa mbele ya Mavho yake. Alisema bila kumumunya maneno, kuwa.... Maaskofu wa ki lutheri alikwisha malizana nao" na kuwa kati ya "Maaskofu wa Kikatoliki 34 wamehongwa Maaskofu 30 na kumtaja kwa jina Askofu Mkuu mmoja, ambaye yeye kapewa fedha za kununulia gari la kiaskofu." Fedha hizo alidai zimetolewa na Lowassa kupitia Rostam Azizi. Gwajima, Tambua kuwa kama ni kweli toka tena hadharani wakemee Maaskofu wanaopokea Rushwa, na kama si kweli Waombe Radhi hadharani Maaskofu hao kwani kauli hiyo ilitaka kuwagawa Maakofu na kuwachafua.

Lakini, alitamka hayo akiona ni sifa, ndiyo maana nilimshangaa kiongozi wa dini ambaye badala ya kukemea anaona ni sifa. Kama wenzangu waliokuwepo na wao wana Misingi ya kusimamia basi watatoa ukweli wao, na kama wanachukia ufisadi basi watatoka hadharani kukemea tamko hilo lililotolewa mbele yetu watu 4 akiwemo Mshenga.

Nilipotamka hivi wengi walidhani Dr. Slaa ndiye Katamka kuwa Maaskofu "Wamehongwa". Kama Askofu anaweza kufika mahali akawasingizia wenzake ni hatari sana na halihitsji kufungiwa Macho na masikio. Kama anavyosema Gwajima ni " kweli". Basi wote tunaopenda kupiga vita Ufisadi ni lazima tupaze sauti zetu, na kukemea kitendo hicho kama kweli kimefanywa na wale tunaotegemea kusimamia maadili katika Jamii yetu. Wako walioniambia Dr. Slaa unapata wapi ujasiri wa kuwasema viongozi wa dini. Sijawahi kuyumba wala kuyumbishwa. Ukweli utatamkwa hata kama ni mchungu, na uovu na uozo utasemwa tu hata kama umetendwa na nani. Ukitazama nyuso za wazi " haki haitatendeka milele.

iv) Katika busara ya kawaida, hatukutegemea Gwajima kujitokeza "Kumkana Lowassa" hasa kabla ya kuomba radhi. Aidha Kauli " Live" kwenye YouTube na mitandao mbalimbali ziko bado kibao. Ama kweli Gwajima ni kiongozi asiye na dhamira kukanusha kauli zake hizo kabla ya kuomba radhi.

v) Wako watakaodhani kuwa Dr Slaa ana "bifu" binafsi na Gwajima. Ni kweli kibinadamu nimeumia sana kwa kuwa kuumizwa na rafiki kunaumiza sana, lakini nawaonea huruma zaidi Watanzania Waliobebwa kwa ushabiki mkubwa na kupoteza nguvu zao nyingi na labda "kupoteza fursa ya kuiondoa CCM kwa muda mrefu ujao" kwa kuwaamini watu kama kina Gwajima. Hiki ndicho kinachonisukuma zaidi kuendelea kumkaba Gwajima hadi atakapoomba radhi kwa watanzania wanyofu.

Nawaomba Watanzania tuwe na kumbukumbu. Tuzisikilize tena Kauli mbalimbali alizozitoa Gwajima, tena wakati mwingine kwa njia ya Maombi kwa jina la Mungu. Hali hii isipokemewa kwa ukali sana ni hatari sana.

Ndugu zangu wanaJF na Watanzania wote,
Pamoja na yote haya, ninawatakia Heri nyingi kwa sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2016 uwe wa Baraka na mafanikio.
By Dr .Slaa

Saturday, December 26, 2015

WALIOMPELEKA MAGUFURI IKULU NI HAWA HAPA

WALIO MPELEKA MAGUFULI IKULU
Kama mtu alikuwa mfuatiliaji mzuri wa mwenendo wa kisiasa katika uchaguzi mkuu mwaka huu atakubaliana nami kuwa wafuatao ndiyo waliompeleka Magufuli ikulu.
1. Watu waliokubali kutukanwa na kudharauliwa kwa kuamini kuwa Magufuli anaweza.
2. Watu waliojitanabaisha ni wa lowassa kwa Watu lakini katika sanduku la kura waligeuka na kuwa wa Magufuli. Na hawa ni wengi kwa idadi ukilinganisha na kundi la kwanza waliojionesha hadharani kuwa wanamwamini Magufuli.
3. Watu walioshituka muda wa mwisho kabisa kuelekea siku ya uchaguzi.
4. Wananchi maskini walioamini kuwa mtu anayefahamu shida zao ni yule aliyeziishi shida hizo. Wanyonge hawa waliweka imani yao kwa Magufuli,,,,hata pamoja na vuguvugu la kutaka kuchoma kitanda badala ya kumtafuta kunguni kukolea wao walibaki na imani yao kuwa Magufuli anaweza.
5.kundi la tano ni kundi la Wananchi walioamini kuwa mabadiliko yanaweza kupatikana ndani ya ccm na kuunga mkono kauli ya lowassa alipokuwa akitangaza nia ya kugombea urais kupitia ccm. Hawa waliamini kuwa chama cha siasa hujengwa na Watu na kuwa kila mtu anahulka na namna yake ya kutenda hawakuamini kuwa eti ccm ya mkapa... Mwinyi inafanana na ya kikwete..... Wao waliamini kuwa kila kiongozi ana namna yake ya kuongoza na kutenda na udhaifu wa kiongozi mmoja huwezi kuwa ni udhaifu wa wanachama wote.
6. Wananchi walioamini kuwa mfumo ni matokeo ya binadamu na binadamu mwenye dhamira njema anaweza kuubadili mfumo mbovu kwa manufaa ya wengi. Hawa waliamini kuwa tabu yetu si mfumo bali ni Watu waliomo ndani ya mfumo yetu kama taifa.... Watu wanaotumia mfumo iliyopo kwa manufaa binafsi.
NINAWAPONGEZENI SANA NYOTE MLIOMPELEKA RAIS MAGUFULI IKULU....... HAKIKA HAMKUBAHATISHA

Friday, December 25, 2015

MATUKIO

WAZIRI NAPE NNAUYE AWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI, KAZI YA KUTUMBUA MAJIPU NI NGUMU NA INA VIKWAZO VINGI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi albam mbili za kwaya ya Wakorintho wa Pili kwenye tamasha la Krismas lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo, ambapo mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini Rebecca Malope amefanya onesho kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi waliohudhuria katika tamasha hili akishirikiana na waimbaji mbalimbali wa hapa nyu mbani na nchi jirani ya Kenya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Nape Nnauye amewaomba watanzania kuzidi kumuombea Rais Dk . John Pombe Magufuli kwa kazi ya kutumbua majipu ambayo amekwishaianza kwani kazi hiyo ni ngumu na ina vikwazo vingi, lakini pia amewataka watanzania na waumini wa madhehebu mbalimbali kuwaombea wasaidizi wake ili waweze kuwa bega kwa bega na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kutekeleza kazi hii kwa ufanisi na kisha watanzania wafaidi matunda na rasilimali zao wenyewe.

Waimbaji kutoka Kenya walikuwa ni Faustine Munishi na Sara K na Solomon Mukubwa kutoka jiji la Nairobi huku waimbaji wa hapa nyumbani wakiwa ni Rose Muhandom Upendo Nkone, Christine Shusho, Edson Mwasabwite, Joshua Mlelwa na wengine wengi, Tamasha hilo pia lilikuwa na lengo la kumshukuru mungu kwa nchi yetu ya Tanzania kufanya uchaguzi kwa amani, Kulia ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWEBLOG-DAR ES SALAAM)
Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo. akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye ili kuzungumza na wananchi katika tamasha hilo kushoto ni Mbunge Martha Mlata na MC Mwakipesile mshereheshaji wa Tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi na mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo katikati ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo na kushoto ni MC Mwakipesile.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiimba moja ya mapambio na kuitikiwa na mashabiki wa nyimbo za injili waliohudhuria katika tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye pamoja na maaskofu na viongozi mbalimbali wakishiriki katika sala maalum ya maombi iliyofanyika katika tamasha hilo,
Wamumini na mashabiki mbalimbali wa muziki wa injili wakishiriki katika maombi maalum ya kumshukuru mungu yaliyofanyika kwenye tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye wakicheza pamoja na mwimbaji Upendo Nkone kutoka kulia ni Mbunge Martha Mlata na Alex Msama wakishiriki kucheza.
 
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Waimbaji wa mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba kwa hisia huku meza kuu pamoja na mashabiki wake wakiwa wamesimama.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Rebecca Malope wakati wa tamasha hilo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Rebecca Malope wakati wa tamasha hilo kulia ni mbunge wa viti maalum mkoa wa mbeya Mary Majelwa na kulia ni Mbunge Martha Mlata.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye pamoja na maaskofu mbalimbali wakiwa wamesimama wakati mwimbaji Rebecca Malope akifanya vitu vyake katika tamasha hilo.
Mwimbaji Christine Shusho na Mbunge Martha Mlata wakiimba pamoja wakati wa Tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye,Alex Msama na Mkewe na baadhi ya wabunge kulia ni Martha Mlata na kushoto ni Mary Majelwa wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya akiiimba katika tamasha hilo.
Wanakwaya wa Wakorintho wa pili wakiimba wimbo wao mara baada ya kuzinduliwa kwa albam zao katika tamasha hilo.
Mwimbaji kutoka nchini Kenya Solomon Mukubwa akiimba na mwimbaji mwenzake kutoka kushoto Sara K. huku mbunge Martha Mlata akishiriki kuimba nao.
Mwimbaji Joshua Mlelwa naye amefanya mambo makubwa jukwaani katika tamasha hilo.

Mwimbaji Rose Muhando pamoja na waimbaji wake wakifanya vuti vyao jukwaani.

BARUA YA WAZI KWA SAED KUBENEA


Mbunge wangu Kubenea achana na siasa za (antagonize) za kina Mnyika, utakuja kimbia Ubungo.

Mbunge wangu Saidi Kubenea, kwanza nakupongeza sisi wote tunaooishi jimbo la Ubungo mbunge wetu ni wewe kubenea na Dk. John Pombe Magufuli ndiye rais wetu.

Kubenea mimi naishi Ubungo makoka kabla ya uchaguzi hukujulikana kabisa huku kwetu Makoka, wengi walikuwa wanamjua Mnyika kama mbunge wetu ambaye anasemwa vibaya kwa kuwa alitutelekeza wana Ubungo na mwisho wa siku akakimbilia kibamba baada ya kushindwa kuyatekeleza aliyotuahidi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Mnyika alishindwa kabisa kuwatembelea wananchi wake na kuwasikiliza shida zetu hususani, kututatulia shida ya maji wana wa Ubungo, kuanzia, mwembe chai, kagera, Agentina, Manzese mpaka Ubungo na kimara yake kwa ujumla, huku nilipo mimi Makoka tulishazoea kuuziwa maji na walanguzi wanapita na magari yao wanatuuzia ndoo shilingi 500 wakati mwingine mpaka sh. 1000.

Mbunge wangu kubenea ukiweza shughulikia hili tunajua wanaotuuzia wanatoa maji katika mabomba ya serikali ukishindwa tutamfata Makonda atusaidie kwa kuwa yule ni kijana mzalendo na asiyetaka masihara akiwa kazini tunajua atawashughuliki
a na tatizo litakwisha ingawa tunajua hupendi kulisikia kabisa jina la mzalendo Makonda.

Mbunge wangu Kubenea nakusihi usiwe kama mbunge aliyetukimbi Mnyika, kama katibu mwenezi wa CHADEMA alitumia muda mwingi kuuza sura katika vyombo vya habari, alifurahia kutangazwa kama mwanasiasa machachari anayeichachafya serikali wakati wananchi wake tunaumia.

Ingawa na wewe umeshaanza tabia hiyo unatumia muda mwingi kushinda makao makuu ya CHADEMA pale ufipa kinondoni, badala ya kutumia muda huo kukutana viongozi wenzako pale makao makuu ya wilaya ya Kinondoni, akiwemo mkuu wa wilaya Paulo Makonda ambaye ni mwakilishi wa rais Magufuli ili msaidiane kutatua kero na changamoto za wana Ubungo.

Mbunge wangu Kubenea tangu tukuchague tumeanza kukuona ukifuata nyayo zile zile za Mnyika za kufuata siasa za kusigana na serikali (to antagonize the establishment) kama anavyofanya Lema kuliko kuwatumikia wananchi.

Mnyika na Lema wanadhani antagonize ni ushujaa, kiuhalisia huo sio upinzani na wala hauna manufaa kwa mwananchi wa kawaida, nakuusia mbunge wangu Kubenea usiige huu upumbafu kazi yako kubwa ni kututumikia wananchi na si kusigana na dola.

Mbunge wangu Kubenea tulipomuwezesha Mnyika kuwa mbunge wa Ubungo mwaka 2010, alikuwa anatumia muda mwingi kukitumikia CHADEMA badala ya sisi wananchi wake tuliyemchagua tafadhali sana usirudie kosa hilo kwani litakukimbiza Ubungo kama alivyokimbi.

Source: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/990047-mbunge-wangu-kubenea-achana-na-siasa-za-antagonize-za-kina-mnyika-utakuja-kimbia-ubungo.html

Rais Magufuli Ashiriki Misa Ya Krismasi Kanisa La Mtakatifu Peter Jijini Dar Es Salmmnnaam Leo


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kushiriki Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015
Sehemu ya waumini katika Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam aliyemkaribisha kusalimia wananchi bada ya kumalizika kwa Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitoa salamu zake za heri ya Krismasi mara baada ya kumalizika Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.