Profesa Lipumba Asema Hana mpango wa kuhama CUF wala kuanzisha chama Kingine ........Ataja Sababu Zilizomfanya Amkatae Lowassa
Aidha
amesema hana mpango wa kuanzisha chama chake kwa kuwa yeye bado ni
Mwenyekiti halali wa CUF kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.
Akiongea
katika kipindi cha Powerbreakfast cha Clouds FM Alhamisi hii, Profesa
Lipumba amesema Katibu Mkuu wa CUF anataka kukiua chama cha CUF Tanzania
bara.
“Mimi nipo CUF bado, na ni Mwenyekiti halali kwa mujibu wa Katiba na sina mpango wa kuhamia chama kingine,”
“Katibu Mkuu wetu anataka chama hiki upande wa bara kife kabisa na ibaki CHADEMA pekee yake ndio maana anafukuza wabunge.,”
“Katibu Mkuu wetu anataka chama hiki upande wa bara kife kabisa na ibaki CHADEMA pekee yake ndio maana anafukuza wabunge.,”
Pia
Lipumba amesema Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif alikosea kumnyima mkono
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein kwa kuwa unapoenda kwenye msiba
jambo la msiba lilipaswa kutawala.
“Hata mimi nilipokutana na Maalim baada ya kunikatalia kurudi kwenye uenyekiti tulisalimiana.” Alisema Lipumba.
Katika hatua nyingine Lipumba alizungumzia sababu ya kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA.
“Sababu
za msingi za kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA, ni kwamba
ukiwa katika siasa unahitaji uongozwe na misingi na ‘principals’ na hoja
kwamba mnagombea kitu gani, na sisi tulianzisha UKAWA kwa kusema kwamba
tutafute nchi, serikali na dola inayowajibika ambayo inatengeneza mambo
vizuri, inatumia rasilimali vizuri itapambana na ufisadi na itajenga
demokrasia ya kweli katika nchi yetu, ukiwa na misingi hiyo kwamba
utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na tulikuwa wote
kwenye bunge la katiba na Mh. Edward Lowassa alikuwepo kwenye bunge hilo
hakuwa mmoja ya wabunge aliyeunga mkono rasimu ya Katiba,” alisema Lipumba.
Alioongeza,
“Kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa na ile misingi iliyotuunganisha
kwamba utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na ukumbuke
Mh. Edward Lowassa alikuwepo katika bunge la katiba ya rasimu ya Jaji
Warioba na hakuunga mkono rasimu hiyo kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa
na ile misingi iliyotuunganisha na kuanzisha UKAWA kuja kumchukua Edward
Lowassa ndiye awe mgombea urais wa watu wanaounga mkono rasimu ya Jaji
Warioba,”