Wednesday, June 29, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya June 29

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya June 29


FELLA ANENA BAADA YA DIAMOND KUKOSA TUZO BET

Mmoja kati ya viongozi wa juu wa label ya WCB, Mkubwa Fella amesema kuwa WCB imekubali kilichotokea katika tuzo za BET licha ya kukiri kwamba walikuwa wanamatarajio makubwa ya kuchukua tuzo hiyo ambayo ilikuchuliwa na Black Coffee kutoka Afrika Kusini.
05diamondtuzo5
Babu Tale, Diamond na Fella
Akiongea na Redio 5 ya Arusha Jumatatu hii, Fella amezungumzia matokeo hayo pamoja na kwanini walikuwa namarajio makubwa.
“Tumepokea vizuri sana kwa sababu mwisho wa siku ni msanii pekee wa Kitanzania,” alisema Fella “Msanii wa kitanzania kuingia kwenye tuzo kama hizo ambazo ni kubwa duniani bado tunaona tunanafasi ya kufanya mazuri zaidi,”
Aliongeza, ‘Hatuwezi sema tulikosea kwa sababu mwisho wa siku yale ni mashindano kwamba mmoja lazima achukue, kwa hiyo Black Coffee alichofanya ulimwenguni kimemeona ni bora, yeye ni bora, kwa hiyo na sisi Watanzania tutengeneze vitu bora kama vya wenzetu,”
Pia kiongozi huyo alisema walikuwa na matarajio ya kuchukua tuzo hiyo.
“Hata ukiniambia leo nikapigane na Tyson na uhakika wa kupigana naye na nikashinda, sina maana kwamba naenda kupigana na Tyson ndio nikapigwe,”

INDIA YALETA SMARTPHONE YA BEI CHEE...BUKU 8 TUU

Kampuni moja ya simu nchini `India imezindua simu aina ya smartphone ambayo itauzwa pauni 2.77 sawa shilingi 8000.
freedom_251_04_ndtv
Freedm 251 ni simu ya Android iliotengazwa na kampuni ya Ringing Bells kutoka India huku ikifananishwa simu ya kampuni ya Apple aina ya iPhone 5.
Ina upana wa nchi nne. Ina programu ya Quad-core inayotoa nguvu ya operesheni ya simu hiyo lakini haitumii betri yake mara nyengine.
Hatahivyo ni vigumu kuipima uwezo wake kwa kuwa ina programu chache ambazo hufanya kazi za kawaiada.
freedom_251_6_ndtv
freedom_251_8_ndtv
freedom_251_5_ndtv
freedom_251_9_ndtv
freedom_251_15_ndtv
freedom_251_2_ndtv

Gesi ya Helium ya Futi za ujazo B ilioni 54 Yagundulika Tanzania

Gesi ya Helium ya Futi za ujazo B ilioni 54 Yagundulika Tanzania


GESI ya helium ya takribani futi za ujazo bilioni 54 inayoelezwa kuwa adimu duniani, imegundulika nchini Tanzania na kuiweka nchi kuwa miongoni mwa mataifa machache yenye madini mengi na muhimu.

Wagunduzi wa gesi hiyo ni watafiti kutoka vyuo vikuu viwili nchini Uingereza vya Oxford na Durham kwa kushirikiana na wataalamu wa madini kutoka nchini Norway.

Watafiti hao wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi hiyo ya barafu, kama inavyofahamika katika eneo la Bonde la Ufa nchini.

Taarifa za waandishi wa habari nchini Japan, zimeeleza kuwa watafiti hao wamesema kuwa uhaba wa gesi hiyo duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari, ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama ‘MRI scanners’.

Pia hutumia katika mitambo ya kinyuklia na katika sekta nyingine nyingi za kiteknolojia.

Wiki iliyopita, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akijibu swali bungeni mjini Dodoma alisema madini yanayotumika kwa ajili ya mitambo ya Apollo na pia vifaa vya matibabu kama MRI na NMR, yamegundulika kuwepo nchini Tanzania.

Hata hivyo, hakufafanua zaidi kiasi cha madini hayo na namna nchi itakavyonufaika na ugunduzi huo. Hata alipotafutwa jana, simu yake ya mkononi ilipokewa na msaidizi wake na kueleza kuwa waziri yuko kikaoni. Madini aina ya helium yanatumika kwa ajili ya mitambo na pia kwenye vifaa vya matibabu kama MRI na NMR.

Kabla ugunduzi huo, watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo ifikapo mwaka wa 2035.

Mnamo mwaka 2010, mwanasayansi ambaye alikuwa mshindi ya Tuzo la Nobel, Robert Richardson alitabiri kumalizika kwa gesi hiyo katika kipindi kifupi. Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu, kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura.

Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, Chris Ballentine alisema gesi hiyo iliyopatikana nchini inaweza kujaza silinda za gesi milioni 1.2 za mashine za MRI.